2017-01-16 15:55:00

Rasilimali maji na changamoto zake!


Kuanzaia tarehe 16 -19 Januari 2017 Falme za nchi za Kiarabu zinakutana ili kujadili kuhusu rasilimali maji. Huu ni mkutano wa tano wa kimataifa mbao utalenga shughuli za kukuza rasilimali endelevu za maji katika muhongo wa dunia, kwenye  maeneo yenye  ukame katika sayari. Wanaoudhuria mkutano huo wa kimataifa ni viongozi  wa kisasa , viongozi wakitaaluma , wataalam wa sekta mbalimbali ikiwemo teknolojia ya biashara. Corrado Sommariva mtaalam katika Teknolojiaa ya mitambo ya kubadili   maji ya chumvi na kuwa ya kawaida kwa  simu huko Abu Dhabi aliongea na  mwandishi wa habari wa Radio Vaticana na kusema Mkutano unahusu  maji kwa sababu katika nchi ya Uharabu, wengi wanafikiri maji siyo rasilimali , na wanategemea karibu wote teknolojia , wakati huo  hata nchi nyingine miongoni mwao wanayo  matumizi yenye kuwa na gharama katika ulimwengu.

Alijibu swali juu ya takafari ya Baba Mtakatifu Francisko katika nchi za Kiarabu kuhusu maji ya kunywa;  akisema kwa upande wa Nchi za Kiarabu mjadala ni mkubwa zaidi kwani tatizo la maji ni limekuwa tatizo la kimataifa kwa ujumla , Yeye binafsi akiwa anashughulikia mitambo ya mabomba ya kubadili maji ya chumvi kuwa ya kawaida anaona kwamba kipengele hiki katika nchi za Ghuba , ni sawa sawa  na mitambo mingine kwa upande wa Japan, China , na India; kwa njia hiyo kuna tatizo kweli la kimataifa ambao maji ni rasimali, na ni kweli  mjadala wenye matatizo kwaajili ya binadamu, ambapo ugavi na usambazaji wake kwa sasa  ni tatizo kubwa na muhimu.

Aidha auliulizwa ni watu wangapi anafikira hawapati maji katika sayari hii ya dunia , na kujibu kwamba siyo rahisi kutoa jibu kamili bali kulingana na umasikini wa dunia hii  yeye binafsi anaweza kukadiria asilimia 50 ya watu duniani wasio  kuwa na maji. Tatizo siyo kwa upande wa upatikanaji wa wingi wa maji, bali masharti na sifa za upatikanaji wa maji hayo yanayokubalika kwa afya ya binadamu.
Hiyo ni kutokana na Shirika la Afya dunia kuweka viwango na tabia ya maji kwa matumizi ya binadamu  kwa afya yake, kulingana na utaratibu huo, kuna mapungufu katika nchi za mashariki ya mbali na nchi za Afrika , ambazo watumiaji wa maji wako mbali na masharti ya sifa zake.
Hali kadhalika Akijibu swali juu ya ufumbuzi wa kutumia maji ya bahari bila kuwa na chumvi:Anasema ya kwamba, njia ya kutumia maji ya bahari baada ya kutolewa chumvi ndiyo njia , lakini lipo tatizo kubwa la kubadili maji ya chumvi kuwa ya kawaida kwani  ni teknolojia ya gharama sana , inatumia umeme mwingi sana; ndiyo maana Mkutano mkuu juu ya Maji  una lengo hilo la kuona uwezekanao endelevu. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.