2017-01-13 16:40:00

Papa asema : ninatambua vema kazi kubwa mliyo nayo na hatarishi


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 13 Januari 2017  amekutana na kuzungumza na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa huduma mjini Vatican.Baada ya ya hotuba ya Kamanda wa Ulinzi na usalama wa Italia wanao endesha shughuli zao mjini Vatican kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi wa Vatican, alitoa hotuba yake  akisema, anayo furaha ya kukutana nao kwa ajili ya kupeana heri za Mwaka mpya ambao kwa muda mfupi umeanza. Pia na kumsalimia kwa namna ya pekee Kamanda wa Kikosi cha walinzi, Daktari  Maria Rosaria Maiorino , akimshukuru kwa maneno ya hotuba yake aliyo itoa. Salam pia kwa wakuu  wote na askari wa vikosi vya ulinzi na usalama.

Aidha alipenda kuwasalimia kila mmoja kwa utambuzi kweli kwa jitihada zao za  huduma  wanazo toa na kusema "matatizo hayakosekani na ni hatarishi.alisema wao ni kama ” malaika walinzi” wa viwanja vya Mtakatifu Petro,kila siku bila kuchoka katika shuguhuguli zenu za kiufundi na ustadi katika kuwajibika kwenu"; na zaidi hasa kwa nyakati hizi za mwisho, mmeonesha  ujasiri kwa  kazi yenu ya kuwajibika katika  kukabiliana na changamoto nyingi na hatari hasa ya kukabiliana na waarifu.Kwa njia hiyo mmeweza kuwasaidia , mahujaji  kuingia kwenye basilika na hata vile kwenye viwanja vya mtakatifu Petro. Kwa hayo yote ninawashurukuru, kwani ninatambaua kazi mkubwa mliyo nayo na sadaka za kila siku ambazo mnakabiliana; na kuongeza jueni ya kwamba ninatambua hivyo na nina wasifu.Mara kwa mara  ninawafikiria kwa dhati na kuwapongeza kwa shughuli hiyo yenye thamani.

Tukio la Maadhimisho ya Jubilei ya huruma ya Mungu kwa miezi ya nyuma  ilifanya mahujaji wafike Roma kwa wingi ktoka pande zote za dunia.Kwa namna hiyo hata iliwalazimu kuwajika sana, ili matukio yote yanayohusu   Jubilei yaweze kufanyika kwa usalama.Ulinzi wenu wa nje ambao mlioufanya kwa kwa uanagalifu na uwajibikaji ulichangia kiasi kikubwa katika mioyo ya ndani ya wanahija , katika kutafuta ile amani ya ndani ya moyo kwa kukutana na huruma ya Mungu. 

Halikadhalika Baba Mtakatifu alisema "tumemaliza muda mfupi kipindi cha Noeli, ambapo kwa mtazamo wetu ulikuwa ni ulikuwa ni kuangalia Yerusalem, nchi ambayo Ndiyo makazi ya Yesu.Kwa mara nyingine Krismasi imetualika tutambue namna  ya kujishusha  kama mwana wake Mungu, ambaye alitaka kujifananisha na sisi, bali pasipokuwa na dhambi, ili tuweze kutambua ni upendo upi wa Mungu alio tupenda.Upendo husio na kikomo, hivyo  ni wito kwetu kuongoka kwaajili ya kuwapokea wengine, kuwapa  mshikamano na upendo kwaajili ya ndugu.Kwa namna hiyo tunaweza kufanya uzoefu wa  amani ndani mwetu kama vile malaika wa Betlehemu walivyo tangaza habari njema".

Na mwishoni Baba Mtakatifu Francisko alisema Mwenyezi Mungu awalinde ili kutumiza shughuli zenu  kwa  ushirikiano na vyombo vingine vya usalama nchini Italia na Vatican. Awaongoze Bikira Maria mama wa huruma, na mama yetu,ambaye ninawakabidhi nyinyi nyote na familia zenu.Nina rudia upya kuwashukuruni kwa kazi zenu mzifanyazo kwa uaminifu; Na msisahau kuniombea!

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.