2017-01-13 16:30:00

Papa amesema: Ili kumfuasa Yesu kikamilifu inawabidi kutembea!


Ili kumfuata Yesu Kristo , tunapaswa kutembea na siyo kubaki tumesimama, “ kusimamisha roho. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa mahubiri ya Ijumaa 13 Januari 2017 katika Kikanisa cha Mtakatifu Martha Mjini Vatican.Baba Mtakatifu akitafakari maneno yaliyosomwa katika Injili ya siku inayo sema juu ya kiwete aliye letwa kwenye kitanda na kushushwa kupitia juu ya  paa la nyumba hadi mahali ambapo Yesu alikuwa amekaa akihubiri watu;kwa tendo hilo Baba Mtakatifu anasema,  imani ikiwa ni ya dhati, inatuweka daima hatarini,lakini tunapata matumaini ya kweli.

Watu wanamfuata Yesu kwa mafao binafsi au kwa ajili ya kupata neno la kitulizo, Papa anasema kwamba hata kama kumfuata Yesu siyo kwa moyo wote, na kwa dhati, lakini muhimu ni kumfua  Yesu, na kutembea nyuma yake.Watu wengi walikuwa wakimfuata kutokana na mamlaka yake na kwa mafundisho yake aliyokuwa akitoa, kwa maneno yake watu walielewa  vizuri, aliponya watu wengi na wengi walikwenda nyuma yake ili wapate kuponywa.Hata hivyo Papa anasema, wakati mwingine Yesu aliwakaripia watu hao walio kuwa wakimfuata ya kwamba hawakwenda  kwa ajili ya Neno la Mungu bali kwaajili ya mambo yao binafsi.

Baba Mtakatifu anasema, “ wakati mwingine watu walitaka kumfanya Yesu awe mfalme kwasababu walikuwa wakifikiri huyo  ni mwanasiasa halisi, lakini watu walikuwa wakikosea, kwani Yesu alikuwa akiondoka zake na kujificha.Licha ha hayo aliacha  afuatwe na wote kwasababu alikuwa ana fahamu wote ni wadhambi". Pamoja na hayo Papa anasema "tatizo kubwa halikuwa kwa wale walio kuwa wakimfuata Yesu, bali ni kwa wale walio kuwa wanabaki wamesimama.Wale waliokuwa wamesimama, maana yake waliokuwa wako pembeni mwa safari na  kuangalia tu, au walikuwa wame kaaa kweli kweli kama vile waandishi,amabao hawakumfuata Yesu, kazi yao ilikuwa ni kutazama na kuchungulia wakiwa juu ya gorofa.Hi ina maana walikuwa hawatembei na katika maisha yao, bali walikuwa wamebwatika katika maisha yao wenyewe.

Daima hawakutaka kuhatarisha maisha yao  bali walikuwa ni kuhukumu tu.Walikuwa wanajisikia ni watu wasio na dhambi na hivyo hawakutaka kuchanganyikana na wengine na   hukumu zao rohoni mwao zilikuwa za kali .Papa Mtakatifu akasema , namna gani watu hawa  hawakuelika, namna gani watu hawa walikuwa ni washirikina ! kwa njia hiyo hata kwa upande wetu ni mara ngapi watu wanatujia na wakiwa ni rahisi, lakini ndani ya vichwa vyetu tua hali ya kujiona , lakini hali hiyo haina sifa nzuri katika Kanisa, alisema Papa.

Baba Mtakatifu alitoa tahadhari ya kwamba watu hawa ni kikundi kilichokuwa kimesimama,kwasababu  walikuwa  juu ya gorofa wakitazama tu na kuhukumu. Hata hivyo  anakumbusha Papa  kwamba "wapo hata wengine ambao wamesimama katika maisha yao, akitoa mfano wa yule mtu, kwa miaka 38 alikuwa karibu na kisima cha maji, amesimama, amekata tamaa  ya maisha ,hakuwa na matumaini na alikuwa ametawaliwa na uchungu wa maisha". Papa akasema "hata huyo ni mmojawapo aliyekuwa amesimama na hakumfuata Yesu pia hakuwa na matumaini".

Watu hao walio kuwa wakimfuata Yesu , baba Mtakatifu  anasema "walikuwa wako hatarini kukutana na Yeye  ili kuweza kupata kile walichokuwa wakitaka.Wanaume walio fungua paa la nyumba walikuwa hatarini:kwasababu mwenye nyumba angewapeleka mahakamani na kutoa mashtaka, ambapo wangelipa. Ni kweli walihatarisha maisha yao, lakini walitaka kwenda kwa Yesu".Pamoja na mfano huo  Papa alitoa  mfano mingine zaidi ,kama wa mwanamke aliyeugua kwa miaka 18 na kwa siri alikwenda  kugusa  vazi la Yesu , hakujali aibu ambayo angeipata  ya kumgusa na ilikuwa ni hatari lakini yeye alitaka afike kwa Yesu aweza kupona.Kwa namna hiyo tufikiri watu wa Kana  kwani  wanawake wa huko wako hatarini zaidi ya wanaume na ni kweli tunapaswa  kutambua hilo. Baba mtakatifu alisema.

Akiendelea na mfano wa huko Kana , Baba Mtakatifu alimtaja hata mwanamake mwingine mdhambi aliye kwenda katika nyumba ya Simon na hata kule Samaria: wote hao walikuwa hatarini lakini wakaokoka. Kumfuata Yesu Papa anasema "siyo jambo rahisi lakini ni vizuri! Daima ipo hatari na mara nyingi ugeuka kuwa kejeri, licha ya hayo   yote neno la mwisho ni kusikia umeondolewa dhambi zako. Pamoja na kupata afya, au tatizo fulani , lakini kuna kupona kwa roho.Kila mmoja wetu anatambua kwamba wote tu wadhambi na ndiyo maana tunamfuata Yesu ili tukutane naye japokuwa tuko hatarini.

Papa alisema, tuepuke roho zilizo kaa tu na kuhukumu wengine kama walivyo kuwa wakimtendea Yesu.Tumfuate Yesu na utambuzi wa kuwa na mahitaji kweli na wakati huo tukitambua hatari iliyopo lakini hiyo ndiyo imani kamili kama vile wale watu waliofungua paa la nyumba na kumtelemsha mgonjwa mbele ya Yesu amponye.Alimalizia kwa swali la kujiuliza kama  tunamwanìmini Yesu katika maisha yetu au nipo ni mekaa nyuma yake na moyo umesimama, umefungwa ulio jaan uchungu na ukosefu wa matumaini ? Ni maswali ambayo kila mmoja anaweza kufanya leo.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.