2017-01-12 15:46:00

Papa asema, tusiwe na kishawishi cha kusubiri kesho bali leo ni leo


Maisha yetu ni leo hii na haitarudia tena siku ya leo. Ni maneno yaliyotamka na Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi 12 Januari 2017 katika mahubiri yake kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha Vatican, akiwashauri watu wasiwe na mioyo migumu,na  bila imani , bali wafungue mioyo yao kwa Bwana. Katika mioyo yetu  kwa dhati kuna mchezo wa "leo" hii: Ni leo hii mkisikia sauti , msifanye migumu mioyo yenu.”Baba Mtakatifu Francisko alianza na sehemu hiyo  iliyosomwa kutoka  katika Waraka kwa Waebrania na kuelezea  mambo mawili muhimu hasa ya “Leo” na “moyo”yaliyokuwa kama ufunguo wa waraka huo.

Papa anasema ni leo hii ambapo Roho  Mtakatifu, katika barua ya waebrania akisema juu ya maisha yetu,kwamba  ni leo iliyojaa siku nyingi lakini ambapo baada ya leo hakutakuwepo na marudio ya kesho, kwasababu ,ni leo ambapo tumepokea upendo wa Mungu. Ahadi ya Mungu tumeipokea leo hii kwasababu tunaweza pia kurudia upya lile agano  kwa uaminifu na Mungu.Lakini pamoja na uwepo wa siku ya leo katika maisha yetu  bado kuna kishawishi cha kusema nasubiri nitafanya kesho.Pamoja na hayo Papa anasema kumbuka kishawishi hicho cha kufanya kesho  ni ile kesho ambayo haitakuwapo tena.

Hiyo ni kama alivyo eleza Yesu kwenye msemo wa wanawali 10 : Papa alieleza, watano walikuwa hawana mafuta kwenye taa zao, na walikwenda baadaye kununua, lakini waliporudi , walikuta mlango umefungwa”.Aidha Papa alitoa mfano mwingine  wa mtu aliye bisha hodi akimwambia Bwana mimi , nilikuwa na wewe, lakini jibu lilikuwa sikujuhi, umefika umechelewa. Papa akasema hiyo ninayo waeleza siyo kwamba ninakutaka kuwaogopesha bali kwa urahisi tu, ni kuwambia juu ya  maisha yetu, yaani  ni kuishi  leo hii: ni leo, zaidi ya leo hakuna tena! na ndivyo ninavyofikiri mimi, papa alisisitiza, na kuendelea;  “ ya kesho itakuwa kesho na  ya daima, isiyokuwa na mawio ya jua ,na itakuwa na Bwana daima na hasa kama mimi leo hii ni mwaminifu.

Papa akitaka watu watafakari zaidi anasema: swali ninalo litoa na hata roho mtakatifu anafanya hivyo: je leo hii ninaishi namana gani ? Akitaka kuelezea juu ya neno  la pili lililotokana na somo , Papa anasema: neno la pili linatokana na somo ni moyo: kwa moyo wa dhati tunakutana na Bwana , ijapokuwa mara nyingi Yesu anatukaripia akisema “ mgumu wa moyo , na ngumu wa kutambua” Wito wake Yesu kutaka kutuonesha jinsi tulivyo na mioyo migumu na tusivyokuwa nai mani kwani tumepotoshwa na dhambi.

Leo hii tafakari  inacheza na  mioyo yetu,  Baba Mtakatifu anasema , je mioyo yetu imefunguka kwa Bwana?, Papa alitoa mfano ya kwamba “ mimi ninashangaa sana ninapokutana na wazee , mara nyingine mapadre au watawa wakiniambia, Baba tunaomba sala zako kwa ajili dakika zetu za mwisho wa maisha yetu . Lakini swali la kujiuliza je kama maisha yako yote umefanya vizuri, kila siku  na huko  katika huduma ya Bwana kuna haja gani ya kuogopa….? Papa anasema , hapana , hapana isiwe hivyo bali  maisha bado hayo hayaelekei  kwenye mawio ya jua, bali inabidi kuishi kiukamilifu ukisali ili leo ifike ukiwa mkamilifu, kwa moyo wa ujasiri na kwa imani bila kuchafuliwa na dhambi,upotofu na  ufisadi.

Kwa njia hiyo, Papa anawashauri kujitafakari  juu ya kuiishi leo hii katika miyo yetu na kusema” leo ni ile iliyo jaa siku nyingi na ambayo haitarudia.Siku zinajirudia hadi mwisho wa Bwana atakapo sema  “inatosha.” Lakini siku ya leo haita rudia tena : maisha ni haya .Na moyo , unapaswa uwe ni moyo uliyofunguka kwa Bwana, usiofungwa na usiyo kuwa mgumu,usiwe mgumu na ukakosa imani, usiwe na shaka , na wala kunuia dhambi .Papa alitoa mfano ya kwamba “Bwana alikutana na watu wengi walio kuwa na mioyo migumu:kama walimu wa sheria, na watu wengine wengi walio kuwa wakimsonga, na kumweka katika  majaribu ili wapate kumhukumiwa … hata hivyo mwisho walifanikiwa kufanya hivyo.

Alimalizia mahubiri yake akisema , leo hii twende nyumbani na maneno mawili : leo hii ikoje ? mawio ya jua  yanaweza kuwa  siku ya leo hii, au ya kusubiri siku zijazo? Je, leo hii ninajisikiaje uwepo wa Bwana? , je moyo wangu umefunguka namna gani? Je niko  imara katika imani? Je ninakubali  niongozwe  na upendo wa Mungu? Kwa maswali hayo, Papa alisema, tuombe Bwana neema ambayo kila mmoja anahitaji.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican .








All the contents on this site are copyrighted ©.