2017-01-10 15:56:00

Papa:Yesu ana mamlaka katika utumishi,na hatoi dharau kwa watu


Yesu alikuwa na mamlaka , na alikuwa anahitaji watu ili apate  kuwahudumia. Yeye alikuwa karibu na watu na alikuwa  mwaminfu katika mafundisho yake, tofauti na walimu wa sheria , ambao walijisikia wafalme. Ni aina tatu ambazo  baba mtakatifu Francisko ameweza kuzionesha katika mahubiri yake asubuhi ya Jumanne 10 Januari 2017 katika Kanisa la mtakatifu Marta. Papa Francisko amesema kwamba walimu wa Sheria walikuwa wakifundisha na mamlaka  ya kikuhani kikuhani, walikuwa wako mbali na watu na pia  walikuwa hawaishi kile wanachokihubiri.

Mamlaka  ya Yesu na ya wafalisayo ni vilima viwili  ambavyo baba mtakatifu ameelezea katika mahubiri  yake , ya kwanza ikiwa ya kifalme na ya pili ya kawaida. Kwani Katika injili ya siku ya Jumanne , ilikuwa inaonesha watu walivyokuwa wameshangaa mafundisho ya yesu , kama mmoja aliye na mamlaka , na wala siyo kama ya mafundisho ya waandishi; ilikuwa ni madaraka juu  ya watu, alisema Papa , kwasababu yale waliokuwa wakifundisha yalikuwa hayaingii moyoni,  wakati yesu alifundisha kwa mamlaka halisi: yeye hakuwa mdanganyifu” alikuwa akifunsidha sheria hadi nukta ya mwisho,” yeye alikuwa akifundisha ukweli na kwa madaraka.

Papa akielezea juu utofauti wao wa mamlaka  ya Yesu na walimu wa sheria , alisema : Yesu alifundisha kwa unyenyekevu kama asemavyo aliye mkubwa katika utumishi ndiye awe ndogo , na mafarisayo walikuwa wakijisikia wafalme. “Yesu alihitaji watu kuwahudumia , alisema baba Mtakatifu kwasababu alikuwa akiwafundisha watu wajue vizuri: na alikuwa mtumishi wa watu. Alikuwa na tabia ya mtumishi , na hiyo ilimpatia mamlaka. Lakini kwa upande wa walimu wa sheria ambao walisikilizwa na watu, walikuwa wakiwaheshimu lakini hawakuwajisikia madaraka juu yao .kwasababu hao walikuwa na saikolojia ya kifalme: ya majivuno, sisi ni walimu na ni wafalme , tunawafundisha ninyi.Hiyo siyo huduma: kwani sisi tunatoa amri na nyinyi mnapaswa kutii".Papa alisisitiza.

Lakini kwa upande wa Yesu hakuwahi kujifanya mfalme: daima alikuwa mtumishi wa wote , na kwa namna hiyo ikampatia mamlaka.Kuwa karibu na watu  hakika ndiyo njia ya mamlaka: Ukaribu ndiyo tabia ya pili inayotofautisha mamlaka ya Yesu na ile ya  wafarisayo. Yesu hakuwa na mgutuko wa watu: kuwagusa  wenye ukoma,wagonjwa, na wala kuwa na kinyaa” wakati mafarisayo walikuwa wakidharau watu masikini , wajinga “, wao wakipendelea kutembea kwenye viwanja wakiwa wamevaa nguo nzuri.

Papa alitoa mfano pia wa ukaribu akisema  yeye anapenda sana kusoma ukaribu wake na  watu  wa Mwenye heri Papa Paulo wa VI akisoma katika Wosia wake namba 68. ya " Utangazaji wa Injili" ('Evangelii Nuntiandi'), na hapo unaona ukaribu wa moyo wa kichungaji: , alisisitiza ni mamlaka ya yule Papa , yaani ukaribu aliokuwa nao na watu.

Alindelea kuelezea utofauti wa wafarisayo na Yesu akisema, hiyo inaonesha jinsi walivyokuwa mbali na watu , hawakuwa karibu; Yesu alikuwa karibu sana na watu na hiyo ilimpatia heshima ya kuwa na mamlaka .Hao walimu wa sheria waliokuwa na umbali na watu , walikuwa na saikoloijia ya kikuhani : kwani walikuwa wakifundisha kwa mamlaka  ya kikuhani yaani kikuhani kikuhani..

Papa aliendela akisema kuna sehemu ya tatu inayotofautisha mamlaka ya walimu washeria na ya Yesu ya kwamba ni ule uaminifu : Yesu alikuwa akiishi kile alichokuwa akifundisha,kwasababu  kulikuwa na umoja , muungano kati ya yale aliyokuwa akiwaza, akisikiliza na kutenda”.Kinyume na  yule anayejisikia kuwa mfalme  tabia yake ni ya ukikuhani kikuhani , maana yake ni mnafiki kwasababu  anasema jambo lakin anatenda jambo jingine.

Matokeo yake  kwamba tabia hizo siyo za uamininfu, na ndiyo maana kwao   kulikuwa na mgawanyiko  hadi Yesu kufikia hatua ya kuwashauri wanafunzi wake akisema, "fanyeni wanayo waeleza lakini msifanye wanayofanya": kwasababu walikuwa wakisema jambo fulani lakini wanatenda kinyume.Hawakuwa wakweli , Papa alisisitiza, na kusema “hiyo ni tabia ambayo Yesu  alisema wazi kwao kwamba ni wanafiki.Hata hivyo inaeleweka wazi kwa yule anayejisikia mfalme au  aliye na tabia ya ukuhani ukuhani, maana yake ni mnafiki ,na  hana mamlaka ! ndiyo asema ukweli lakini hana mamlaka. Tabia hiyo ilikuwa kinyume na Yesu kwani yeye  alikuwa mnyeyenyekevu ,mtumishi na yuko karibu na watu, ambaye pia  hakudharau watu, ni mwaminifu na alikuwa na mamlaka. Ndiyo mamlaka wanayohisi watu wa Mungu.

Kwa kumalizia mahubiri yake ,ili kuelewa  vizuri juu ya mahubiri hayo aliwakumbusha injili inayo simulia msamaria mwema aliye mwokoa yule mtu aliyepigwa na kuachwa na maharamia karibu ya kufa na kusema , "alipita kuhani , akamwona na kupita mbali akifiri huyo mtu amevuja damu , nikizigusa nitatakuwa mchafu, , akapita mtu wa pili Mlawi, Papa akasema" akafikiri akipitia pale atajichanganya kwenda mahakamani ili kutoa ushuhuda , na wakati mimi ninayo mambo mengi ya kufanya, na huyo akawa amekwenda zake.Na mwisho wake akatokeza msamaria , na mdhambi , lakini mwenye kuwa na huruma .Pia Papa akasema kuna hata mtu mwingine katika nyumba ya mapokezi, ambaye lanada alibaki kwa mshangao mkubwa, siyo kwaajili ya mtu aliye na majeraha , maana alikuwa amezoea kuona vituko hivyo vikitendeka barabarani, na hata  wale watu wawili, Kuhani na Mlawi ambaye bilashaka alikuwa akiwafahamu bali alimshangaa Msamaria. 

Mshangao huo ulikuwa ni wa maswali ya hivi huyo ni mwenda wazimu, kwasababu hakuwa ni Mhebrania, bali alikuwa ni mdhambi, Papa alisema kwamba huyo mtu angeweza kufikiria hivyo.

Kwa kuelezea zaidi Injili ya siku ya Jumanne 10 Januari 2017 Juu ya mamlaka ya Yesu ambayo ni yenye unyenyekevu na utumshi, na mamalaka yaliyo karibu na watu na uaminifu,  Papa aliunganisha hata Injili hiyo ya msamaria mwema ili kuelewa vema juu ya mamlaka ya Yesu.

 

Sr Angela Rwezula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.