2017-01-10 16:15:00

Papa:Ujumbe wa utume wa sala kwa mtandao wa mwezi Januari 2017


Baba Mtakatifu Francisko katika nia zake za jumla kwa Mwezi Januari 2017 anasema  tusali kwa ajili ya: kwa  ulimwengu wa sasa, wakristo wengi katika makanisa yanayo toa huduma ya binadamu wenye mahitaji , wanaotetea maisha ya binadamu na utu wake, kwaajili ya mazingira na  kupinga uonevu wa kutokuwa na haki. “Utashi wa kutembea kwa pamoja na kushirikiana  katika huduma  na mshikamano dhidi ya wadhaifu na wanaoteseka ni sababu ya furaha kwa wote”. “Unganisha sauti yako katika sala yangu ili wote wapate kuungana  katika sala kwa upendo wa maombi ya  umoja wa Kanisa  katika huduma kwenye changamoto za binadamu.

Aidha katika toleo la kwanza 2017 , Video ya mwezi Januari ya Papa Francisko inatoa wito wa kuombea  “ Wakristo katika changamoto za kibinadamu” na anawatia moyo waamini wawe na minajili ya kufanya kazi kwa pamoja katika kutoa huduma ya kibinadamu na hasa wale wahitaji, kwa maana hiyo ni kuungana naye katika mitandao ya kijamii katika sala ya dunia. Tarehe 9 Januari 2017 : Video ya Papa imefikia toleola 13 na hivyo , video hiyo ni mwendelezo wa sehemu ya pili ya video ya kila mwezi kwaajili ya kuamsha hamu ya binadamu katika utume wa Kanisa.


Lengo kubwa la nia ya sala ya Baba Mtakatifu Francisko katika mitandao ya kijamii ni kutaka kuonesha changamoto hizo za kibinadamu zilizopo , na hivyo Papa Francisko anaomba watu waweze kuwa na mshikamano wa umoja wa makanisa ili kila mwezi watu wewe na ufahamu wa mahitaji makubwa ya sala. Tangu 2016  ilivyotokea  video imetazamwa na watu karibia milioni 13 na imekuwa  chanzo pia  cha kuhariri makala 4,000  yaliyotolewa  na magazeti ya  kimataifa na  katika lugha zaidi ya 10.Kwa mujibu wa takwimu rasmi  za Kipapa za mwaka mjini Vatican, asilimia 31% ya idadi ya watu duniani ni Wkristo, na kati yao asilimia 17,7% ni wakatoliki.


“Ni katika imani na ushuhuda , ni katika maisha halisi ya kila siku tunapojitafakari  ile hamu ya umoja wa Wakristo.Kutafuta namna ya kutembea kwa malengo ya umoja na ni jambo la haraka”, Papa anasema: Kuungana kwaajili ya Sala na kutoa sadaka ya huduma ni changamoto katika dunia hii, lakini ni jibu bora zaidi tunalo weza kutoa kwa Bwana Yesu kama alivyokuwa akisali kwa moyo wake wote na kutuachia ushuhuda wake; “naomba ili wote wawe kitu kimoja. Baba naomba wawe ndani yetu  kama vile wewe ulivyo ndani  yangu , nami ndani yako. Naomb wawe kitu kimoja kusudi ulimwengu upate kuamini kwamba wewe ulinituma.” "(Yh 17, 21),"

Hata hivyo katika Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili 8 Januari 2017 Baba Mtakatifu aliwaalika watu wote kuuungana na mtandao wa utume wa sala iliyowasambazwa kupitia mitandao ya kijamii , ambayo ni sala itolewayo kila mwezi kwa Kanisa zima , ili kuendelea mbele katika utume wa sala unaowafanya Wakristo kushikamana na kukua katika umoja.” Alithibitisha hayo Padre Frédéric Fornos, SJ Mkurugenzi wa kimataifa wa Mtandao wa Utume wa Sala  na matawi yake ya Vijana wa Mshikamano wa Ekaristi.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radi Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.