2017-01-07 15:06:00

Mwaka 2016 umekuwa ni wa kuvunja rekodi ya wahamiaji nchini Italia


Mwaka 2016 umekuwa mwaka wa kufunga  rekodi kwa wahamiaji zaidi ya 181,000 waliofika kwenye fukwe za Italia. Hiyo ilidhibitishwa na Shirika la Frontex la  Umoja wa nchi za  Ulaya linaloshughulikia mipaka ya nje , baada ya ripoti za kwanza kutolewa na na Serikali ya Italia. Ripoti inasema kwamba hiyo ni idadi ambayo haijawahi kurekidiwa ambako  umoja wa Ulaya wameiita “mapambano katikati ya bahari ya Meditrenia, kwa ongezeko la asilimia 20% ukilinganisha na idadi ya mwaka 2015.


Ongezeko la waliofika Italia kutokana na Shirika la Ulaya linaloshughulikia mipaka ya nje, linafanya kutafakari juu ya ongezeko la wahamiaji  na hasa waliotoka  katika Bara la Afrika ,na zaidi Afrika ya  mashariki.Pamoja na ongezeko hilo kwa upande wa wahamiaji waliofika Ugiriki wanaripoti wamepungua kwa asilimia 79% , kufikia 182.500.


Kwa ujumla Shirika la Frontex linakadiria kuwa mwaka 2016 walifikia watu 507.700 hao  waliovuka mipaka kwa ukiukaji wa sheria na kuingia nchi za Umoja wa Ulaya na kati yao 364.000 kwa kupitia njia ya bahari.  
Wakati huo huo , Tume ya Ulaya inasema inapokea uamuzi wa serikali ya Italia ya kutaka kufungua majengo ya ziada kwaajili ya utambulisho  na kuwarejesha makwao wahamiaji walioingia kinyume cha sheria.


Lakini kwa upande wa nchi ya Italia suala hilo limezua mzozo na utata kwa mapendekezo yaliyo tolewa na Waziri wa Mambo ya ndani Marco Minniti wa kutaka kufungua vituo kwaajili ya utambulisho na kuwafukuza walioingia bila kinyume na sheria, pia  kwa upande wa makubaliano ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa kuangalia kwa upya namna ya kuwagawanya wanaoomba ifadhi katika sehemu zote nchini italia.

 

Sr Angela Rwezaula 

 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.