2017-01-06 14:58:00

Ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Armenia huko Aleppo


Kiongozi Mkuu  wa Kanisa la Armenia na mtume wa Kilikia Catholicos Aram I aliamua kufanya ziara yake huko Aleppo wakati wa sikukukuu ya Krismasi , mahali ambapo kuna família nyingi zilizo lazimika kuacha nyumba zao na kukimbilia katika nchi nyingine.

6 Januari 2017, kiongozi huyo  Aram I aliadhimisha misa Takatifu katika Kanisa la Mama wa Mungu , na baada ya misa hiyo alikutana na waamini  wa Armenia.Tarehe  7 Januari 2017 Catholicos anategemea kutembelea majengo ya Kanisa na Jumuiya mbalimbali, na mchana wa siku hiyo hiyo atatembelea Kanisa la Utatu Mtakatifu la liturjia ya Armenia,ambapo atakutana pia  na Askofu Mkuu Miryati katoliki wa liturjia ya Armenia huko Aleppo.

Na mwisho atamalizia ziara yake kwa kutembelea katika Kanisa la Kiinjili  kutoka  Armenia huko Aleppo .Taarifa zinasema kwamba hata hivyo kabla ya kufanya ziara yake, tarehe 4 Januari 2017  Aram I alikutana na Rais Bashar al Assad wa Damasko.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.