Madaraja ya mshikamano kati ya Italia, Camerun na Syria kufanywa na vyama mbalimbali visivyo vya kiserikali kwaajili ya kumsaidia mwanadamu wa sasa anaye endelea kuteseka na hali ya maisha, na vyama hivyo ni kama ifuatavyo:Chama cha Patrizio Paoletti kwa ushirikiana na New Life for Children na Amal kwaajili ya Elimu wamezindua mradi wa Elimu katika eneo la Kills , kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.Mradi huo umepokea watoto karibia 45,000 wakiwa wanakimbia kutoka eneo la Aleppo.
Kazi ya wanachama hao wamejikita katika mitaala ya shule katika ulimwengu, na lengo
lao ni kutoa msaada wa vifaa vya ufundishaji kwa elimu na kwa wahudumu wa kituo cha
elimu “Bayt Al Amal””maana yake nyumba ya matumaini. Utaratibu huo ulioundwa na Amal
kwa Elimu, kwaajili ya kuwasaida watoto na watu wazima wakimbizi wa Syria waweze kuwa
na kutuo cha maisha ya kijamii na elimu.
Hayo yalielezwa na mhusika mkuu wa Chama cha Paoletti, Bwana Marco Benini juu ya dhamira
ya miradi na mipango ya kijamii inayofanywa na vyama hivyo.
AFRIKA
Tukigeukia sehemu ya pili ya ni kwa upande wa Afrika , mahali ambapo inasemekana
“ kuwa na mtoto mlemavu ndani ya familia ni kama vile umeadhibiwa na walemavu hao
hawana maisha mema ya baadaye kwasababu ya kubaguliwa au kutelekezwa.Hayo ni maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa shirika la kutoa huduma lisilo la kiserikali la DOKITA ,Bwana
Mario Greco akisema; lakini pamoja na hayo vituo vya afya vyenye uwezo wa kusaidia
watoto wenye mahitaji maalumu , ki ukweli ni vichache sana na vinagharimu sana.Pamoja
na kugharimu,bado kuna sababu nyingine ambayo mara kwa mara familia nyingi nazo zinachangia
zenyewe kuwaondoa au kuwaficha watoto walemavu , kwa kasumba ya utamaduni wa kuwazia
kwamba watoto hao wamelaaniwa mbinguni au kwasababu ya rasilimali za kiiuchumi kuwa
ndogo.
Camerun ni moja ya nchi za Afrika inayosemekana kwamba kuna matukio mengi ya ulemavu kwa watoto,ni asilimia 23% ya wenye umri kati ya miaka 2 na 9 wanaishi na mmoja akiwa na ukosefu wa akilli, na mara nyingi imetokana na magonjwa kama vile malaria , ukoma , surua na zaidi kinachodhofisha ni utapiamlo.
Ili kutoa jibu halisi la ukosefu wa huduma za afya kwa watoto walemavu na yatima
, Huko Kusini mwa Camerun , ni zaidi ya miaka 35 , shirika la kutoa huduma ya kibinadamu
isiyo ya kiserikali DOKITA ilianzisha vituo kadhaa maalumu. Kati ya hivyo ni “Foyer
de l’Esperance, a Sangmelima”, ni mashirika ambayo kila mwaka wanatoa huduma ya matibabu
na mazoezi ya watoto walemavu wapate kupona na pia pia huduma ya ukaribu wao kwani
ni zaidi ya watoto 6,000 na vijana wenye ulemavu.
Muhusika Sista Laura Figueroe , mmisionari wa shirika la watoto wa mama Maria mkinngiwa
wa dhamabi ya Asili akiwa pamoja na shirika la DOKITA ni kitovu cha maisha kwa mamia
elfu ya watoto” maalum”
Ili kusaidia huduma ya mtawa Laura na "Foyer e L’esperance", tangu tarehe 8 hadi 28 Januari 2017 , Shirika lisilo la kiserikali la Dokita limezindua Kampeni iitwayo “Wote ni sawa”.Ni kwa kutuma fedha kwa njia ya ujumbe wa sms kwenye namba ya mshikamano 45519 ,fedha zitakazo kusanywa zitatumika kununua vifaa vipya kwaajili ya tiba ya viungo vya mwili , na kwaajili ya kufunga maabara.Michango hiyo pia itasaidia katika mtaala wa elimu na hasa kwaajili ya elimu ya msingi kwa watoto wenye kuwa na mahitaji maalum na kwa miradi mbalimbali ya kuendeleza jamii, kiuchumi , kutamaduni kwa vijana wanye ulemavu.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |