2017-01-06 13:43:00

Caritas Italia kujikita katika tatizo la umaskini na wanyonge


Ripoti ya mwaka 2016 ya Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki nchini Italia  Caritas, wakati ikiwa inasheherekea miaka 45 tangu kuanzishwa kwake, na umekuwa mwaka wa ushirikiano wa Caritas majimbo na wadau wake wa mikoa na mashirika mengine ya kimataifa kujitikia katika tatizo la hali ya umaskini na  wanyonge nchini Italia Ulaya na katika ulimwengu. Katika mwaka 2016 ambao umekwenda sambamba na mwaka wa Jubileo ya huruma na iliyofungwa 20 Novemba 2016 , Caritas kwa kipindi chote cha mwaka walishirikiana bega kwa bega na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali ya MISSIO NA FOCSIV katika kampeni iliyokuwa inaitwa “ haki inapaswa kubaki katika uzalendo"

Kwa fursa ya tukio la mwaka wa huruma pia waliandaa na kushirki Kongamano la Caritas ya majimbo Kitaifa , lililofanyika huko Sacrofani Roma kuanzaia 18 hadi 21 Aprili 2016 , na siku ya kumalizika kwa komgamano hili wapata kukutana na  na Baba Mtakatifu Francisko katika ukumbi wa Paulo VI wakiwa ni , wawakilishi wote wa Caritas za majimbo nchini  Italia.Kwenye mkutano huo na Baba Mtakatifu  alitoa msisitizo wa mwendelezo wa utume wao ya kuwa ni  kwaajili ya huduma ya  Kanisa kwa watu na hasa  wale maskini zaidi na walio baguliwa.

Pamoja na hayo yote waliyoyafanya Caritas kwa mwaka 2016, hata mwaka huu inabidi kukabiliana na kipeo  kwa pamoja katika utume wa kupambamana na changamoto zinazoikabili nchi na zaidi umaskini, kwasababu inakadiriwa milioni 4 na 598,000 sawa sawa na asilimia 7,6% ya watu wote nchini Italia ni maskini. Kutokana na tatizo hili linaloikumba nchi, Caritas ya  Italia ilitoa taarifa kwenye ripoti mbili: ya kwanza ikiwa ni sera za kisiasa katika kupinga umasikini nchini Italia iliyokuwa na kauli  “ hatusimami mbele ya sheria".

Na sehemu ya pili ya ripoti ya mwaka 2016 juu ya umasikini na ubaguzi wa jamii ikiwa na kauli “Vyungu vinawasiliana”. Na hiyo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza waliweza kukabiliana na  matukio  yenye urefu na upana wake, hasa kwa kutazama upeo wa Taifa ,wakitafuta mwafaka wa kupata kielelezo cha kuunganika kwa pamoja katika kukabiliana na hali iliyopo ndani ya nchi, pia zile zinazojitokeza katika milango ya nchi.

Pia  Caritas ya Italia ilikuwa ni kutafakari kwa umakini kwa upande wa vijana katika nchi  kwa maana hiyo ni  (vijana wanaosoma, wanaofanya kazi, na wale wanaotafuta ajira) na hasa wale waolifika wao moja kwa moja kwenye vituo vya Caritas au kwa kutumia wazazi wao.  Kwa mtazamo huo, wakati wa kumaliza mwaka 2016 Caritas ilitoa wito kwa Taasisi zote za kiraia na akiwemo Rais wa nchi ya Italia na Rais wa Bunge kwa kuomba ipitishwa sheria ya kuanzisha  ushirikishwaji wa Mapato (REI) na kuweka mipango wazi ya kitaifa juu ya kupinga umasikini na uwekezaji uwe kwaajili huduma ya kweli ya jamii.

Wakitafakari zaidi Caritas kwa mwaka 2016 wamegusia juu ya suala la wahamiaji kutokana na utafiti wa toleo la 25 wa  ripoti ya "Caritas Migrantes" na ripoti ya 3 juu ya ulinzi kimataifa , kwa ajili ya kukabiliana na msongamano wa wahamiaji, ili kupata majibu hasa ya kutafuta nafasi za kuwapokea .
Lakini pamoja na harakati hizo na mipango hiyo mingi ya Caritas ya Italia , kwa mwaka jana , ni pamoja na dharura  kubwa iliyojitokeza ya tetemeko la ardhi la 24 Agosti 2016 iliyokumba sehemu ya mikoa ya kati na kusababisha vifo vya watu 300 .

Caritas ilianza mara moja kutoa huduma na mshikamano wao kwa watu waliopata maafa hayo kwa kupitia wawakilishi wa Caritas walioko katika maeneo hayo.Kwa makusanyo ya fedha  kitaifa tarehe 18 Septemba 2016 zilipatikana euro milioni sita. Taarifa hiyo ni kutaka kuonesaha namana gani Caritas ya Italia imejishughulisha katika huduma ya dharura kwa binadamu, ambapo kwa mwaka 2017 bado inataka kushika hatamu kwasababu ya kuitikia wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa mara ya kwanza ameweka adhimisho la siku ya masikini duniani, itakayoadhimsihwa kila Jumapili ya 33 ya mwaka wa kawaida ambapo Baba Mtakatifu alisema "tunapaswa kuandaa sikukuu ya Yesu Kristo Mfalme wa Ulimwengu, ambaye amejitambulisha kwa watu maskini, na yeye atatoa hukumu kulingana na matendo ya huruma". Aidha "Ni siku ambayo itamfanya kila mbatizwa atafakari juu ya umaskini , a ndiyo moyo wa injili, kwa maana haiwezekani kuwapo haki na amani ya jamii endapo Rasaro ataendelea kuwapo katika milango yetu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.