Habari kutoka kwenye Gazeti la Oservatori Romano , linatoa kisa cha wanawake wa Eritrea kufungwa huko Libya na kuwa waatihirika mara mbili. Kisa hicho kimetokana na vijana au watu wengi kiacha nchi zao wakifikiri wataweza kujikomboa kimaisha wakiingia katika nchi nyingine lakini matokeo yake ni kama haya anayosimulia kijana wa kike wa Eritrea.
Wered ni msichana wa miaka 16 kutoka Eritrea alikuwa na ndoto ya maisha yake ya
baadaye ya kwenda Ulaya , akifikri angesoma, baada ya masomo angepata kazi, baadaye
angetengenza familia.Ndoto hizo pia zilikuwa baada ya kazi ataanza kuwatumia ndugu
zake fedha za matumizi .
Baada ya mwaka mmoja na nusu kupita aliamua kuondoka na kile alichokuwa amekwisha
kusanya na kuwacha familia, mama yake huko Eritrea. Alianza safari na kukatisha nchi
ya Sudan hadi nchi ya Libia, fedha alizo kuwa nazo zilikuwa ni kuwapatia wafanya biashara
haramu ya binadamu ili apate nafasi kwenye mtumbwi wa kuvumsha bahari ya Meditrenia(Bahari
ya kati) na kufikia fukwe za Lampedusa nchini Italia.
Mawazo yote hayo hayakufika mbali bali,kwani safari yake ilishia mpakani wakati wa
ukaguzi kwenye kituo kimoja Ajdabja Libia ya mashariki, ambayo ni sehemu mojawapo
yenye kupitiwa na wakimbizi wengi wanapokuwa wakielekea forodha ya Tripoli.
Mpakani hapo kijana huyo alitekwa nyara na kikundi cha wanaume akiwa pamoja na kikundi
cha mwanawake zaidi ya 10 waliokuwa wakiongozana na safari yao ya kutafuta maisha,
na kupelekwa kwenye forodha za Sirte.Forodha hizo zikumbukwe ni forodha alikozaliwa
na kifo chake aliyekuwa rais Ghedafi.Kwa mwaka mmoja sehemu hiyo ilitangazwa kuwa
Serikali ya kiislam ya Isis, mji mkuu wa Tripoli.
Leo hii msichana Wered anao ujauzito , lakini hajuhi ujauzito huo ni wa nani kutokana na kwamba, yeye na wenzake wameingizwa kwenye kwenye biashara ya ngono na wanajeshi wa Al Baghdad huko Libia. Akihojiwa na mwandishi wa habari, Wered anasema "ameuzwa" anayasema hayo akiwa amefunikwa uso na kitambaa cha dhambarau, lakini kwenye macho yake inaonesha kweli mateso yake na mahangaiko.
Kijana anasema kutokana na kutokujua huyo mtoto ni wana nani na wala hajuhi ni miezi mingapi ya ujauzito , mtoto huo hamataki na kutamka “ ni mtoto wa shetani” na kuendelea, "kwa miezi minne nimeuzwa kwa wanaume wa nne. Mpaka sasa ninaye mmoja wa nchi ya Sudan, ninachotamani tu ni kusahau , tamani kusahulika kabisa, kusahau nilivyotumiwa kama jalala, kusahau nilivyo uzwa mara walipochoka kunitumia"
Aidha kijana wered alitoa ushuhuda wa vitendo vya vingi na vya kutisha vinavyoendelea
kuwapata na mateso makuu akiwa na wenzake kutoka Eritrea.Jinsi gani walivyoshurutishwa
kuukana ukristo , wakielezwa na watesi wao ya kwamba wamepata kuwakata shingo wakristo
wengi kutoka katika nchi yao, na kama hakubali kubadili dini yao nao wataishia kukatwa
shingo mbele ya watu na kuwachoma.
Walikuwa wakikimbia umasikini, lakini leo hii wako kifungoni , wanakuwa waathirika mara mbili, hawawezi kufikia lengo lao, ndoto yao ya kufika Ulaya, licha ya hayo hawezi pia kurudi makwao kwasababu wanasema upo uwezekano wa kuwawa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |