2017-01-02 15:03:00

Siku ya kuzaliwa kwa Bwana , tuwakumbuke wanaoteseka na tupeleke amani


Kusheherekea sikukuu ya Noeli ni utume wa kimisionari kwa wakristo  na kuwa waaminifu wa kuendeleza ukuu wa utume wa kimisionari unaonesha upendo wa Mungu kwa jirani na hasa kwa watu wasikini. Hayo yalikuwa ni mahubiri ya Askofu Mkuu Gabriel ‘Leke Abegunrin wa Jimbo kuu la Ibadan wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Oke Padi Ibadan. Katika mahubiri yake Askofu Mkuu wa Jimbo la Ibadan, alisema upendo mkubwa, huruma na unyenyekevu wa Yesu kristo ambaye ni Mungu, aliyefanyika mwili na kuzaliwa katika pango, umekuwa utume wa waamini wote  kuwasambazia watu wote kwasababu tunaiga tunachoiga kutoka kwake nasi tunapaswa  kupokeana kuwatangazia wengine.

Askofu Mkuu alindelea kusema, “ kuna fursa nyingi, ambazo katika taifa letu  , kwa namna tunavyoishi , vinatufanya tuwe na dharura kwa ajili wakristo wote,  na hasa kile ambacho Yesu alituletea amani kwa wakati ule na hivyo ni kuwa na amani kati ya watu. Amewataka watu wakati huu;  kuwakumbuka watu wengi wanakwenda kulala usiku wakiwa na njaa, watu wasio na makazi, watu wasio kuwa na vituo vya afya , watu wanao shinda na ndoo zao wakitafuta maji na hata  wale walio na pweke   kwasababu ni wagonjwa , wanasumbuka na hali zao za maisha kama vile wazee.

Kwa namna hiyo aliendelea na wito wa kuwaonya ya kwamba;"kuwa waaminifu na kuangalia  kile kinachowazunguka hasa kwa upande wa usalama:chuki na manunguniko wakati mwingine siyo ya kweli, ubinafsi au  kupenda kutumia hovyo" aliwawahimiza kwamba, ili kuwa mwaminifu lazima  kuishi kiroho na kuwa macho , waangalifu, subira, kama vile alivyokuwa Yesu wakati wote wa maisha yake.  Kadhalika Askofu Mkuu aliwaonya  Wakristo wasiwe kikwazo kwa mtu yoyote , ya kutokujali au kujiingizaa katika vitendo vya   ushirikina , na wasitoe nafasi ya  migogoro ndani ya mioyo yao na katika maisha yao.

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.