2017-01-02 15:34:00

2017 ni mwaka wa maparokia nchini Ufilipini


"Mwaka wa maparokia, muungano wa jumuiya”ndiyo itakuwa kaulimbiu iliyochaguliwa na Mkutano wa Baraza la maaskofu wa Ufilipini kwa mwaka 2017.

Tamko hilo lilitangazwa hivi karibuni  wakati kuanza matayarisho ya kusheherekea miaka 500 ya uinjilishaji katika nchi yao itakayofanyika 2021.

Akieleza hayo Rais wa Baraza la maaskofu la Ufilippini (Cbcp) Askofu Mkuu  Socrates Villegas alisema maparokia ni jumuiya ndani ya  jummuiya yenye chemichemi ya kimisionari na mwamko wa uijilishaji mpya, ambao unataka maisha ya kimisionari, ni kama  alivyosema hata baba Mtaktifu Francisko ya kuwa Parokia siyo Taasisi iliyo kitu bure , bali inafanya mang’amuzi makini na ambayo utegemea mwamko wa kimisionari na uwajibikaji wa Paroko na Jumuiya.

Ikumbukwe kwamba katika kuadhimisha sikukuu hiyo kwa mwaka 2021, ni miaka 9 Kanisa la Ufilipini linaendelea na mandalizi hayo yaliyoanza tangu 2013 sambamba na mwaka wa Imani ulitangzwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI ,na mwaka kati ya 2013 na 2014 walitafakari juu ya mafundisho kamili ya imani kwa  uwajibu wa walei, ambao ni“watendaji wa uinjilishaji.”Mwaka 2015 ulihusu masikini, na mwaka 2016 walitafakari juu muungano kati Ekaristi takatifu na familia ikiwa sambambamba na kongamano la kimataifa la Ekaristi Takatifu iliyofanyika huko Cebu mwishoni wa Januari 2016.

 

Baada ya Mwaka 2017 ambao ni mwaka wa maparokia, itafuata tafakari juu mapadre na vijana watakao ongoza miaka miwili ya 2018 na 2019. Mwaka 2020 Baraza la maaskofo wa ufilipini watatafakari kuhusu njia ya kiekumene na majadilianio ya kidini katika kuhamasisha “ thamani ya amani na maelewano na hasa katika seheme zenye migogoro. Na mwisho 2021 utakuwa ni mwaka wa utume kwa mataifa(“missio ad gentes”), ili kila mwamini awe na msukumo wa kuwa mmisionari”.

 

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.