2016-12-30 15:39:00

Yaliyojiri katika maisha na utume wa Papa Francisko 2016


Mwaka 2016 umekuwa ni matukio makubwa katika maisha na utume wa Papa Francisko. Baba Mtakatifu Francisko kwenda sehemu zilizofanyika  mauaji ya kimbari  huko Uholanzi  (Auschwitz) na ya huko Lisbon (Hispania), kutangazwa kwa  Wosia wa  Kitume ya  Furaha ya Upendo ndani ya familia na bado Papa alikutana na Patriaki Kirill na kutembelea Lund kwa tukio la kusheherekea miaka 500 ya Mageuzi ya Kiluteri Duniani na  maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu , hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyojiri kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa mwaka wa 2016
 
 Ili kupata maelezo kamili  juu ya matukio haya ya Baba Mtakatifu na ni jinsi gani alivyoyaishi kwa kipindi cha mwaka huu, Alessandro Gisotti Mwandishi wa Radio Vatican, alimuhoji Padre Antonio Spadaro Mkurugenzi wa Gazeti la "Civiltà Cattolica", kwa mtazamo wake wa matukio hayo ya Baba Mtakatifu, naye alipta ya kueleza kwamba "Anaamini kupembua  vipindi viwili  kwa upande wa Baba Mtakatifu kwamba kwake yeye ilikuwa  ni kupambanua na huruma. Na kwamba  “kwa upande wa huruma inahitaji mabadiliko,ikiwa hayo ni mabadiliko ya ndani. Mabadilko ya Kanisa , mabadiliko ya kitume , na utume wa Papa ambaye ametafuta namnakutekeleza  ndani ya Kanisa tangu  mwanzo  wa utume wake.Hata hivyo aliendelea ;utume wake aliuelezea sana  hata katika Wosia wa Kitume wa Papa wa  Furaha ya Injili  (Evangelium gaudium).

Halikadhalika Huruma ni kutambua  maana yake, ya kwamba hakuna lolote linaloweza kututenganisha na upendo wa Bwana ambaye amekuwa karibu nasi daima na ambaye daima anatusubiri. Hivyo basi ni kuonesha uso wa Mungu kwa kizazi cha leo ambacho kwao wanaonekana kuwa mbali kidogo, kama vile kioo cha gari kilichofunikwa na mavumbi. Huruma maana yake ni   milango ya Mungu na Kanisa daima imefunguliwa .

Mwandishi wa habari aliuliza swali :  mbele ya matukio ya mauaji ya kimbari  na mateso  ya huko Lesbos, Sweden,  Poland, Auschwitz, na kwa maeneo ya tetemeko la ardhi  Italia, Baba Mtakatifu Francisko alichagua ukimya , nini maana ya ujumbe wake ? Padre Spadaro alijibu : “Baba Mtakatifu hapendi kuelezea uchungu, kama jinsi nilivyotambua mimi ya kwamba hapendi kutoa hukumu kwa Mungu bali ni kuonesha ya kwamba Mungu yupo daima na binadamu anayeteseka; kukaa kimya maana yake ni kuwa karibu na mtu huyo na  tuseme  ni aina ya dawa. Jambo alilofanya papa , analifanya hata kwa watu wengi, mfano tuliona hata alipokuwa kwenye kuta za  Bethlehemu, na Poland (Auschwitz), kwahiyo ni kusema anabembeleza mateso ya madonda  na hiyo ndiyo maana ya kuponya,Hata hivyo ndiyo maana ya Msalaba wa Kristo, yaani kujitwisha uchungu na mateso anayoishi binadamu. Hiyo  siyo kimya kitupu bali kimejaa ukaribu wa dhati.

Swali jingine lilikuwa “Juu ya Wosia wa Kitume wa Papa Francisko juu  Furaha ya Upendo ndani ya familia uliyotangazwa mwaka huu, ambayo ilijitokeza hata lawama, na mabishano kwa upande wa wakatoliki . Ni namna gani Baba Mtakatifu aweze kukabiliana na lawama hizi? Padre Spadaro alisema mara kwa mara Baba Mtakatifu amesema misukosuko ni sehemu ya maisha , na hivyo ni muhimu hata kwa mchakato wa Kanisa. Tuseme baba Mtakatifu naweza kuwa  na wasiwasi iwapo hakuna jambo linalotendeka au pasipokuwa na upinzani. Kwahiyo kama mchakato huo ni dhahiri basi unaunda matokeo ya ari halisi.Hata hivyo Wosia wa Baba Mtakatifu wa Furaha ya Upendo ndani ya familia  ni muhimu kwasababu inajikita katika historia siyo tu kwa watu wa Mungu bali kwa kila mwamini kwenye mahusiano binafsi na Mungu. Kwahiyo  wosia huo unamfanya binadamu  ajitafakari na kwamba anavyojisikia na hisia zake ya kuwa  familia ni kiini cha msingi wa jamii ya sasa.

Aidha  Wosia huo wa kitume unazo sehemu mbalimbali Lakini  sehemu ya familia  ni kama kiini, licha ya uwepo wa  nyufa, na migogoro, lakini inatafakarisha ya kwamba  Mungu yupo  katikati ya historia  ya imani yake. Kwa  namna  hiyo ujumbe wa Wosia huo  unawaalika hata makuhani, wote kuwa karibu na kila historia ya mtu binafsi.

Na mwisho lilikuwa swali: Ni jambo gani unafikiri limekuwa nyeti kwake kwake Baba Mtakatifu  kwa kipindi cha mwaka huu na pia wakati wa kusheherekea miaka 80 ya Kuzaliwa hivi karibuni , kitu ambacho labda yeye hakugundua. Padre Spadaro anajibu ya kwamba ni vigumu  kutambua  kwani zipo sehemu nyingi  katika utume wake, pamoja na kwamba haikukosekana misukosuko kwa kipindi chote .Labda jambo ambalo nimelitambua mwaka huu ni ule utulivu wake alio nao .Baba Mtakatifu daima ni mtulivu, na anatambua mapema tukio lolote linaljitokeza karibu yake , hata yale ambayo ambayo yasingempendeza.

Yeye mwanyewe alisema anakula vizuri, analala vizuri ; Padre Spadaro akaongeza "na ninaweza kuongeza  anasali sana. Na kwa njia ya msingi  wa sala ndani ya Mungu unamfaya awe na utulivu wa hali ya juu,  jambo ambalo kusema kweli lanishangaza"

Sr Angela Rwezaula

Idhaa Ya Kiswahili Ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.