Katika tukio la kufunga mwaka , Msimamzi mkuu wa Nyumba ya kipapa , ametoa takwimu ya mahujaji walioweza kufika kwenye matukio mbalimbali yaliyoendeshwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican kwa kipindi chote cha mwaka 2016 ambapo watu 3.952.140 wameudhuria matukio hayo : Matukio haya yanaunganisha matukio makuu, maalumu, matukio ya Jubileo ya mwaka wa huruma , maadhimisho ya liturjia Takatifu, sala za malaika wa Bwana na katika sala ya Malkia wa Mbingu. Lakini ikumbukwe kwamba , taarifa hizi za karibunini ambazo zimehesabiwa kutokana na tiketi zilizotolewa na wasimazi wa nyumba ya kipapa, ambapo zinajumuisha, namba ya waamini walioweza kudhulia vipindi vya sala ya malaika wa Bwana au Sala ya malkia wa mbingu zilizofanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro.
Zaidi ya hayo, takwimu zinaonesha miezi ambayo watu walikuwa wengi kama vile mwezi
wa tatu, kutokana na uwepo wa Juma Takatifu na pia Mwezi wa Septemba kwenye tukio
la kumtangaza Mama Theresa wa Calcutta kuwa Mtakatifu, na kufanya idadi ya watu 3.952.140.
Takwimu hiyo inaonesha mikutano na iliyofanyoka Vatican tu , kwa namna hiyo haionyeshi
idadi wa maudhulio ya matukio mengine ya Papa aliyoweza kufanya ziara yake ya kichungaji
katika majimbo ya Roma na Italia kwa ujumla.Pia haionyeshi hata ziara za Kimataifa
za kitume kama inavyosemekana kwamba Baba Mtakatifu alikutana na mamilioni ya watu
kwenye maadhimisho ya misa Kakatifu , ikiwa ni pamoja na watu wengi waliokuwa njiani
wakimsubiri apite kwa mfano (Mexico. Lesvos Ugiriki , Armenia, Poland, Georgia, Azebaigian
ma Sweden.)
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican.
All the contents on this site are copyrighted ©. |