2016-12-30 16:35:00

31 Desemba 2016 filam ya Jubilei ya 2016 ya Papa Francisko kuoneshwa


Tarehe 31 Desemba 2016 , itaonyeshwa , filam ya Jibileo yenye ujumbe wa ” Njia ya msamaha”, iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Mawasiliano mjini Vatican. Filamu hii ni kazi iliyofanywa kwa ushirikiano kati ya Radio Vatican na Kituo cha Televisheni cha Vatican, taasisi ambazo kuanzia tarehe Mosi, Januari 2017 zinaunganishwa na kuwa taasisi moja chini ya Sekretarieti ya Mawasiliano. Filam hiyo ni mkusanyiko  wa sehemu mbalimbali za matukio ya maadhimisho ya Jubilei kuu ya huruma ya Mungu iliyofungwa hivi karibuni pamoja na maadhimisho ya Jubilei nyingine zilizofanywa na Mama kanisa kama sehemu ya mwendelezo wa historia, maisha na utume wa Kanisa!

Filamu hii inaonesha kimsingi historia ya maadhimisho ya Jubilei mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa tangu mwaka 1300, kimsingi matukio haya ni sehemu ya historia ya binadamu inayoendelezwa na Mama Kanisa katika maisha na utume wake! Filamu hii inasisimu na ina mvuto na mashiko kwa wasikilizaji na watazamaji wake; imeandaliwa kwa ufundis, utaalam na weledi kwa kutumia ufundi na teknolojia ya kisasa, ili kuonesha ubora wa matukio ya maadhimisho ya Jubilei zilizopita na hizi za wakati huu. Maana ya filam hiyo ni kuonesha hatua mbalimbali muhimu za historia ya jubilei  kwani ni tukio ambalo lilianza tangu 1300 na ambalo limejirudia katika historia  ya Kanisa na kwa maana hiyo ni Historia ya binadamu.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.