Baba Mtakatifu Francisko katika katekesi yake ya kila Jumatano, na iliyofanyikia katika ukumbi wa Paulo wa sita tarehe 28 Desemba 2016 , ametoa tafakari juu ya imani na matumaini ya Abrahamu baba wa imani kutoka (Mw 15, 3-6). Alianza kusema , katika Barua ya Mt. Paulo kwa warumi , inatukumbusha sura ya Ibrahimu baba wa imani , kwa kutuelekeza njia ya Imani na matumaini. Mtume Paulo anaandika , “Abrahamu aliamini na kutumaini na hivyo amekuwa baba wa mataifa mengi kama maandiko matakatifu yasemavyo “wazao wako watakuwa wengi kama nyota” (Rm 4,18). Mtakatifu Paulo anaonesha namna Ibrahimu alivyo amini Neno la Mungu, ahadi ya kupata mtoto. Na hiyo ni imani kubwa ya kuamini kuzidi kiasi cha matumani hayo. Kwasababu ni jambo ambalo lilikuwa kinyume na hali yake alivyokuwa, kwasababu yeye alikuwa tayari mzee na mke wake alikuwa mgumba.
Kwa kuamini ahadi hiyo Abrahamu alianza safari , na kukubali kuacha nchi na mali zake na kuwa mhamiaji, akiwa na mategemeo ya jambo “lisilowezekana” ahadi ya Mungu ya kumpatia mtoto, pamoja na kuwa mke wake alikuwa tayari ni mgumba na mzee. Abrahamu aliamini na imani yake ikamfungulia matumaini, na kuongeza, ukifikiria kwa mtazamo wa kijujuuu jambo hili halina maana , kwasababu inaonekana kweli ni jambo lisilo wezekana. Papa aliendelea , lakini matumaini hayo yana fungua upeo , na kukuwezesha uote hata jambo ambalo haliwezekani na hata kufikirika. Matumaini yanakufanya uingie gizani wakati usiotegemea ili upate kutembea kwenye mwanga.
Lakini hiyo ni safari ngumu, papa alisema , kwani kuna kipindi ambacho hata Abrahamu alipata wasiwasi na kukata tamaa. Lakini aliendelea kuamini hadi kufikia nchi aliyokuwa ameelekezwa na Mungu,japokuwa muda ulizidi kupita bila kumpata mtoto , na tumbo la Sara lilibaki na ugumba wake.
Papa aliendelea “ ndipo Abrahamu alianza kulalamika kwa Bwana; “Ee mwenyezi Mung utanipa nini hali naendelea kuishi bila mtoto, na mrithi wangu ni Elizier wa Damasko: Tazama hujanijali mtoto ; mtumwa aliyenizalia nyumbani mwangu , ndiye atakuwa mrithi wangu. Ndipo Mwenyezi Mungu akamtokea akamwambia Hapana mtoto huyo hatakuwa mrithi , bali yule aliyezaliwa na wewe ndiye atakuwa mrithi”
Na hapo mwenyezi Mungu akamleta nje na kumwambia tazama juu angani zihesabu nyota
kama unaweza kuzihesabau, na kuongeza …. huo ndiyo utakuwa urithi waki ..Na yeye akaamini
Bwana alivyo mwambia kwa haki (Mw 15,2-6)
Papa akachambua hilo na kusema, tukio hilo lilifanyika wakati wa usiku na nje kuna
giza , na hiyo ina maana hata katika moyo wa Abrahamu , kuna kukata tamaa, kutokana
na matatizo ya kuendelea kuamini kile kisichowezekana. Hiyo ni kwababu baba huyo ameshakuwa
mzee wa miaka mingi , na kwamba jamabo hili lisingewezekana kuwa na mtoto, bali anayebaki
ni mtoto wa mtumwa kuchukua urithi wake.
Hata kama Abrahamu yupo anaongea na Bwana wakati huo, lakini bado bado uwepo wa Bwana
siyo kitu unafanana kuwa mbali naye, kwasababu hajaweza kutimiza ahadi ya neno lake
. Abrahamu alijisikia upweke , ni mzee, amechoka na , kifo kinamkaribia. Je ni namna
gani aendelee kuamini?
Papa anabainisha kwamba hata hivyo malalamishi hayo ni namna ya kuishi imani.Pamoja
na hayo yote Abrahamu aliendelea kuamini Mungu na kutumaini chochote bado kinachoweza
kutokea.
Papa aliuliza ni kwasababu gani Abrahamu anaendelea kulalamika , na kutafuta ahadi
hizo?, Ni kwasababu , imani siyo kusema ni ukimya tu na kutufanya tukubali bila mabishano
ndani ya mioyo yetu, au matumaini siyo jambo la uhakika wa kukufanya usiwe na mashaka
au wasiwasi, bali Imani ni mapambano na Mungu ya kumuonyesha uchungu wetu bila kijificha.
Matumaini vilevile siyo kusema yanakuondolea hofu ya kuangalia hali jinsi ilivyo,
bali ni kukubali hata majaribu hayo.
Baba Mtakatifu alisema Abrahamu kwa imani yake anaelekeza maombi yake Mungu ili
aweza kumsaidia aendelee kutumaini. Na Bwana alimjibu kwa msisitizo wa ahadi yake,ya
kwamba, mrithi hatakuwa mtoto wa mtumwa , bali atakuwa mtoto wake manyewe atakayetoka
katika uzao wake.
Hakuna chochote kilichobadilika kwa Mungu kwasababu yeye aliendelea kurudia ahadi
yake aliyo tamka tangu mwanzo, na siyo kwamba anamtokea ili Abrahamu aweze kujiskia
uhakika. Uhakika wake alio nao ni ule wa kuamini neno la Bwana na kuendelea kumtumainia.
Ishala aliyo mpatia Abrahamu ni kama sala ya kuendelea kuamini na kutumainia kile
alichomwambia “ hapo mwenyezi Mungu akamleta Ibrahimu nje na kumwambia “Tazama
mbinguni , zihesabu ; Hivyo ndivyo wazao wako watakavyokuwa wengi.”(Mw 15,5) Baba
Mtakatifu alieleza jambo hilo lilikuwa bado ni ahadi na ambayo alipaswa kusubiri
kwa wakati ujao.
Aidha Baba Mtakatifu alisema nini maana ya hema akisema; Mungu alimpeleka Abrahamu
nje ya hema , ina maana ya kumtoa katika maono yake finyu , na kumuonyesha nyota;
aliongeza, ili kupata kuamini, inabidi kutazama kwa macho ya imani; ni nyota tu
ambazo wote tunaweza kuona , lakini kwa Abrahamu nyota hizo lazima zigeuke kuwa ishala
ya uaminifu wa Mungu.
Na mwisho akasema baba Mtakatifu , Na hiyo ndiyo imani , ndiyo njia ya matumaini ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuikimbilia. Iwapo hata sisi tutakuwa na fursa ya kutazama zile nyota , utakuwa ni muda wa kumwamini Mungua na hakuna jambo lililo zuri zaidi ya hilo.
BAADA YA KATEKESI YA PAPA
Baada ya Katekesi yake Baba Mtakatifu aliwasalimia watu wote hasa kwa namna ya pekee
vijana, wagonjwa, na wana arusi, akisema leo ikiwa Kanisa linaadhimisha Sikukuu ya
watoto mashahidi , kwa ,aombezi yao wapate kuwasaidia wote kuwa na nguvu ya imani
, na kumwangalia mtoto wa Mungu , ambaye kwa fumbo la kuzaliwa kwa Bwana amejitoa
kwa binadamu wote.
“Vijana wote mtambue ya kwamba mnakua kama yeye na hivyo ni kuwatii wazazi na kuwa
tayari kutambua na kufuata utashi wa Baba aliye mbinguni”.
Akiwageukia wagojwa baba Mtakatifu aliwatakiwa matashi mema ya sikukuu hizi za kuzaliwa
kwa Bwana na hasa wao waweza kuangazwa na Mwanga wa Betlehemu , na kutambua maana
ya mateso yao.
Vilevile wanandoa alisema waweze kudumisha kila siku na kujenga familia zao kwa upendo
na kujitoa sadaka zaidi.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |