“Kanisa linawapokea wale wanaopenda kumkaribia Mungu wakati wa Sikuu ya kuzaliwa
kwa Bwana” Ni utangulizi wa Maneno ya Padre Sergio Ticozzi Mmisionari wa Pime Huko
Hong Kong China akitoa ushuhuda wa watu wake wakati wa mahojiano na mwandishi wa
habari wa Radio Vatican juu ya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana.
Anasema; Kwa kawaida China wanasheherekea sikukuu kwa namna ya pekee, kwasababu ni
watu wengi wanakwenda kanisani, haijalishi hata kama idadi kubwa siyo wakatoliki na
wala wakristo.Wanakwenda kwa kujisikia wana mahitaji; Ni mahitaji ya kiroho ya kukutana
na Bwana , kwa njia hiyo ni fursa kubwa kwa Kanisa la Chiana kukutana na watu hawa
walio na utashi wa dini , kwa imani yao katika Bwana.
Aidha alisema sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana imeangukia muda mfupi wa kumalizika mwaka
wa huruma, ambao umekuwa mwaka wa aina yake, kwani umeleta maridhiano ya watu kwa
Bwana , ya ndugu , ya jumuiya na ndani ya familia.
Halikadhalika kwa upande wa Hong Kong, ushuhuda wameweza kuutoa kwa njia ya jumuiya
ndogo za kiparokia ambao wamekwenda kuwatembelea wagonjwa hopitalini, katika nyumba
za wazee , na pia vituo vya walemavu kwaajili ya kuwapelekea zawadi ndogo na kusali
nao kwa kutumbuiza nyimbo… huu ni mshikamano wa kuweza kushirikishana furaha ya Noel
, ambayo ndiyo maana yake, alisema Padre Sergio.
Na hii ni kutokana na mwaka huu kwa namna ya pekee wa mwaka wa huruma ulikuwa na
vigezo vya matendo ya huruma na kwa njia hiyo umewafanya watu kuwa na msukumo na mwamko
wa kufanya matendo ya huruma ya kuwasaidia wenye shida , waliobaguliwa , wagonjwa
na walio na upweke.
Akiongelea juu ya matatizo yalipo katika Kanisa la China alisema kuwa ni kumwachia yote Bwana anayeweza kugusa mioyo : wanachofanya wao na jumuiya zao ni kumuomba Bwana awafanye waendelee kuwa chombo cha amani katika mikono yake, na mwisho wake hasa wapate kuwa tayari kukabiliana na vishawishi vya ulimwengu huu vinavyojitokeza.
Halikadhalika wawe tayari kufungua miyo yao kiroho kwaajili ya maelewana na watu wengine , katika jumuiya , na kuishi kwa maelewana ndani ya familia na ndani ya jamii. Hayo ndiyo matazamio ya msingi wa watu wa Hongo Kongo na China.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |