2016-12-24 15:41:00

Wasiwasi wa Wakristo nchini Misri bado upo, ulinzi unahitajika


Baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Kanisa Kuu Katoliki la kikopta nchini Misri,  Mons. Kyrillos Willian, Askofu Katoliki wa Kikopta wa Asiud amendika katika Gazeti la Shirika la Kipapa kwa ajili ya Msaada kwa Kanisa hitaji, juu ya hali halisi inayoendelea katika Jumuiya za Kikristo huko Misri, akisema mashambulizi ya hivi karibuni ya kigaidi  yamewalete maafa makubwa na uchungu sana wakristo. Na akasema, Jumanne 20 Desemba 2016  idaidi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia  26 kutokana na  kifo kingine cha mtoto wa miaka 10 aliyekuwa amejeruhiwa kwenye shambulio hilo; hata hivyo  Askofu William anatia moyo wa matumaini ya watu akisema “pamoja na hayo ipo hali ya watu kuwa na matumaini kwa Mungu .

Hiyo ni kama vile zamani makundi ya uhaini walikuwa wakishambulia waamini wasiweze kwenda kwenye maeneo yao  aidha alielezea ,Askofu  juu ya mshikamano kutoka kwa  watu wasiokuwa wakristo ya kwamba “wanatoa misaada ya hali na mali, kuonesha ushirikiano , na pia  viongozi wa Serikali walianza mapema kutafuta wakosaji, ikiwa hata  Rais  wa Misri A-Sis  alitamka ya kwamba asingeweza kuudhuria hata mazishi iwapo wasingekuwa wamewapata wahusika na tukio hilo, na kuongeza Askofu William “ hii ina maana yake kwetu” kuona Rais uwepo wake kwenye  mazishi na kuwapa kila mmoja mkono wafiwa ,na viongozi wawakilishi wa Kanisa.

Hata hivyo pamoja na yote hayo, wasiwasi na hofu  bado ipo na hasa kwa  siku kukuu za kuzaliwa kwa Bwana kwasababu Isis imetangaza.
Kwaajili ya ulinzi wa Jumuiya za Kikristo, Monsinyo William alieleza ,” Viongozi wahusika , wametuomba ushirikiano, pamoja na kwamba ni shughuli yao kwa kuwalinda raia wao lakini , wanataka pia kuwafundisha watu wetu namna ya kukaa chonjo, na pia kwa vijana wetu maskout ambao mara nyingi ufanya ulinzi wakati wa Ibada za misa,watapatiwa  mafundisho yanayo husu ulinzi wa raia. Mitambo ya ulinzi imeshawekwa tayari mbele ya Kanisa kuu , na sehemu za kulala wageni.

Sr Angela Rwezaula.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.