2016-12-24 16:14:00

Siku kuu ya Mtakatifu Stefano Shahidi: Mshikamano na wanaoteseka


Wakatoliki nchini Ujerumani wanaalikwa Jumatatu, tarehe 26 Desemba 2016, kuadhimisha Siku ya Sala kwa ajili ya wakristo wanaoonewa  na kubaguliwa sehemu mbali mbali sanjari na Siku kuu ya  Mtakatifu Stefano ambaye ni mfiadini wa kwanza kikristo. Kanisa la Ujerumani limeeleza, kwenye ibada ya siku hiyo, sala za maombi zitalenga  juu ya kuwaombea  ndugu dada na kaka  katika imani duniani wanaondelea kwa kimya kuteseka na kubaguliwa na hasa wazo kuu hasa litawendea wakristo wote  nchi za Uarabuni, wanao lazimika kuishi imani yao mafichoni. Halikadhalika,  taarifa Kutoka ofisi ya Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Ujerumani, linasema wametengeneza vifaa muhimu vya kutumia kama mabango na picha kubwa za kubandika kwenye madirisha , ya maparokia, ikiwa ni kuipa maana siku hiyo katika mshikamano wa Kanisa wa sala kwaajili ya ndugu hao wanaoteseka.

Pamoja na maandalizi hayo ya siku ya sala,  kuna agizo moja muhimu kwa wanajumuiya wote mahalia  kwamba wakumbuke wako katika sikuku ya kuzaliwa Bwana , hawana budi kuwa na shagwera ya sikukuu hizo paomoja na kukumbuka wakristo wanaoteseka. Historia ya utaratibu wa siku ya sala kwa ajili ya kuonesha mshikamano kwa wakristo wanaoteseka na kubaguliwa kwa nyakati zetu , ulianzishwa mwaka 2003 na Baraza la Maaskofu Katoliki Ujerumani. Kwa miaka 13 hivi sana , shughuli hizo kwaajili ya makanisa yaliyo kimya na matatizo yao, imeendelezwa na Kanisa Katoliki la Ujerumani.

Sr Angela Rwezaula.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.