2016-12-23 15:13:00

Maaskofu DRC kuongoza mchakato wa majadiliano ya kisiasa!


Askofu mkuu Marcel Utembi Tapa, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Jamhuri ya Kidemokrasia  ya Congo (DRC) alitoa wito kwa vyama vya upinzini kufanya mazungmzo na makubaliano  kwaajili ya usimamizi wa kipindi cha mpito  ,hayo  ni kwasababu ya kutaka suluhisho la   mgogoro wa kisiasa nchini humo kutokana na Rais wa nchi hiyo  kumaliza muda wake. Aliyasema hayo wakati wa kumalizia kikao cha Baraza la Kitaifa la Viongozi wa Kidini la Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo CENCO, linalosimamia upatanishi kati ya serikali na upinzani, na kutoa pendekezo la kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo Alhamis 21 Desemba 2016.

Nia ya  Maaskofu wa Kanisa la Katoliki, wanatafuta namna ya kuweza kutatua mizozo iliyopo ndani ya nchi, kwani hadi hivi sasa tofauti kuu iliyopo ni juu ya mamlaka ya Rais Joseph Kabila wakati wa kipindi cha mpito, baada ya muda wake rasmi  kumalizika 19 Desemba mwaka huu. Vyama vikuu vya upinzani vilivyoungana chini ya jina jipya la Rasemblement walisusia mazungumzo yaliyoongozwa na Umoja wa Afrika,na kutaka serikali ya mpito ikiwa itaongozwa na Kabila au la ni lazima ipunguze sana madaraka ya kiongozi huyo. Halikadhalika upinzani unataka uchaguzi ufanyike mnamo mwaka ujao wa 2017, huku serikali na baadhi ya vyama vya upinzani vinataka uchaguzi ufanyike 2018.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.