Undishi wa habari ni taaluma iliyo hatari , leo hii ni nchi nyingi duniani kote,
si tu katika maeneo ya vita yenye Serikali za kimabavu , bali pia katika mazingira
juu ya karatasi, na demokrasia.
Hii ni Ripoti ya mwaka ya Shirika la Waandishi wasiokuwa na Mipaka, wenye makao Mjini
Paris Ufaransa na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari mjini New York.
74 wafanyakazi wa vyombo vya habari wamepoteza maisha yao ikiwa , 57 ni waandishi
wa habari, 9 ni wanablogu na 8 wasaidizi wa vyombo vya habari kwa mwaka 2016, na
hiyo ni sababu ya utendaji wao wa kazi wa kutoa taarifa tu. Sehemu kubwa wa waandishi
wa habari waliopoteza maisha katika sehemu za vita :19 Siria, 10 Afghanistan, 7 Irak
na 5 nchini Yemen.Lakini katika nafasi ya tatu kwenye orodha ya mstari mwekundu kwa
uchapishaji ni nchi Amerika ya kusini katika nchi ya Mexico ambapo 9 ni waathirika
wa tukio hilo. .
Shirika la Waaandishi wasio kuwa na Mipaka wanalalamika kuwa kuna mapengo ya kweli ya maelezo japokuwa waandishi wa habari 780 wamepoteza maisha yao kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita wakiwa wanatafuta hali halisi na siyo tu ya vita vinayoendelea ,bali juu ya uhuru na ukiukwaji wa haki, rushwa, vitu ambavyo ni changamoto na ni kipigo hata kwa nchi nyingi za kidemokrasia.
Kutokana na takwaimu kwa mfano nchi ya Italia kwa upandewa wa Shirika la Ulaya la haki za binadamu zinaonesha, miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2016, 92 yamekuwa ni matukio ya vitisho, mashinikizo na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari,ikifuatia nchi ya Ufaransa ambayo ilipata matukio 95.
Mwaka 2016 vilevile umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa kufungwa jela waandishi wa habari
, kama isemavyo Kamati ya ulinzi wa Waandishi wa habari (CPJ) Ni waandishi 256 walioko
ndani ya magerreza za Serikali. 81 wakiwa nchini Uturuki, na zaidi ni waandishi 38
walioko magereza ya China, ikifuatiwa na nchi tatu za Afrika ambazo ni Misri , Eritrea
na Ethiopia. Mbali na waandshi hao , bado waandishi 40 waliopotea au kutekwa nyara
katika Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini.
Sr Angela
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |