Baadhi ya viongozi wa Kikristo wa Bangladesh walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani na kuomba serikali kuhakikisha usalama wa Wakristo wakati wa kipindi cha sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na Waziri aliwahakikishia ulinzi wa polisi kwa makanisa 62 katika mji mkuu.
Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani huko Dhaka, na wawakilishi
25 wa Muungano wa Makanisa ya Kikristo .Naye Rais wa Muungano wa Wakristo Nirmol
Rozary aliliambia shirika la habari la AsiaNews akisema ,"walikutana na waziri huyo
na walimpelekea heri na salamu ya sikuu ya kuzaliwa kwa Bwana kwa niaba ya Jumuiya
zote za Kikristo.
Aidha akielezea hali hiyo aliendela na kusema ,wasiwasi wa wakristo unatokana na hali
ya kutokuwa wavumilivu wa wageni kutoka nchi za nje walioko katika nchi na hasa Mapadre,pia
Jumuiya ndogo za Kikristo na wahindu.Kiongozi huyo wa Wakristo aidha alimuomba waziri
mambo ya ndani kuhakikisha uwepo wa umeme bila kukatika watakapokuwa wanasali misa
za sikukuu .
Na kwa upande wa Waziri Asaduzzaman Khan Kamal aliwahidi kuwa hatakikisha hatua zaidi za usalama zinatekelezwa nchini kote wakati wa sikukuu za Noel na mwaka Mpya, na kuongeza ya kuwa tunao wasiwasi juu ya ulinzi wa Wakristo , polisi wetu watakuwepo katika makanisa yaliyopangwa kwenye vipindi hivyo vya sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana
Mji wote utadhibiti makanisa 62 na kuahkiksha kwamba nchini kote unawekwa mifumo ya
ufuatiliaji wa mitambo ya kulinda na pia kuzuia foleni za magari kupitia barabara
ya maeneo ya Ibada za kikristo.Hata hivyo Serikali imewataka pia wakristo wasifanye
sherehe kwa kutumia milipuko ya fataki .
Huko Bangladesh wakristo ni wachache, asilmia 0,6% ya milioni 160 ya wakazi.Na Jumuiya
ya wakristo iliyo kubwa ni ile ya wakatoliki, ambao wanakaribia waamini 600,000.
Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |