2016-12-21 15:52:00

Vita na matumizi ya nguvu kamwe hayakuweza kuleta amani na haki, bali vifo na vurugu


Vita na matumizi ya nguvu kamwe hayakuweza kuleta amani  na haki , bali zaidi ni kuleta vurugu, vifo na uharibifu, hayo yalitamkwa na Na askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa katika mkutano na waandishi wa habari juu ya tukio la sikuku ya kuzaliwa kwa Bwana Jumanne 20 Desemba 2016  huko Yerusalem, na Mons. Pizzaballa ni msimamizi wa kitume wa nchi Takatifu huko Yerusalemu.


Msimamizi huyo alisisitizia juu ya kutaka wafanye mazungumzo  ya kisiasa na kupata na ufumbuzi  kwani aliendelea “Jeshi linaweza kushinda vita , lakini katika ujenzi inahitaji sera za kisiasa, na sisi hatuoni , na maisha ya wengi yako hatarini katika mchezo wa vita, na mwisho wake masikini na wanyonge ndiyo wanaotoa  gharama kubwa.”.


Katika hotuba yake msimamizi wa Kitume Yerusalem alitoa mfano  miongoni mwa jumuiya za wakristo wa misiri , kwamba wanaishi chini ya vitisho , kama ilivyodhibitisha katika mashambulzi ya hivi karibuni katka Kanisa la kikopt mjini Kairo.Aidha na kusema, hata sisi ni sehemu ya uwajibu, kwani hatuwezi kuendelea kuongea  daima juu ya  mazungumzo , haki na mani. Maneno matupu hayatoshelezi, tunatakiwa kupambana kwaajili ya  umasikini na haki ,  kwa kutoa ushuhuda  wa huruma.”


Hali kadhalika alisema  juu ya mashambulizi ya nchi kuanzia Yordania ambapo Jumapili iliyopita ilitokea mashambulizi ya kigaidi huko Karak na kusema hata huko virusi vya magaidi vimeingia kwani siyo habari mpya , ni lazima kufanya kazi sana hasa  katika  sehemu ya elimu na maendeleo, la sivyo hata katika sehemu hiyo vijana nao watajifunza ugaidi kama wao.


Askofu Mkuu pia alilaumu  juu ya ukosefu wa maono, ya nchi ya Israel na wapalestini ambao kwa muda mrefu wamekosa mazungumzo na dhamira dhabiti ya amani na kusema  ni jambo ambalo watawala wanapaswa kuliangalia kwa haraka na kwa  ujasiri , kwaajili ya kusaidia watu wao wanaokabiliwa na hali ngumu na wanazidi kuomba amani.

Sr Angela Rwezaula 

Idhaa ya Kiswahili ya radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.