2016-12-20 15:37:00

Watoto 47 waokolewa huko Aleppo


Tarehe 19 Desemba 2016 watoto 47 waliokuwa wamenasa kwenye kituo cha watoto yatima huko Mashariki mwa Aleppo waliokolewa na wako salama ingawa wengine wana majeraha. Uokoaji wa watoto hao ni sawa na maelfu ya watoto ambao wamekwisha okolewa kwa siku zilizopita . Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Geert Cappelaere aliyasema hayo 19 Desemba 2016, akieleza kuwa wengine wanakabiliwa na ukosefu wa maji mwilini;na kwamba  wanachofanya sasa kwa kushirikiana na wadau ni kusaidia kuwaunganisha watoto hao na wengine waliookolewa hivi karibuni kuungana na familia zao.

Halikadhalika kuwapatia huduma za haraka za matibabu na nguo za baridi zinazohitajika ikiwa bado kuna habari kuwa wengi wao katika mazingira magumu.UNICEF imekumbusha pande zote na ziwe na  majukumu yao chini ya sheria za kimataifa ya kuwalinda watoto, popote pale walipo.

Vilevile  nchini Italia , wametoa   wito juu  ya maandalizi ya siku ya Aleppo 22 Desemba 2016 .Hii ni kwaajili kuhamasisha  raia il  kutambua hali ya watoto wa Aleppo na Siria wanavyoendelea na mgogoro ya kivita. ”Tunapaswa kuvunja ukuta wa kutokujali ambao unandelea kufunika vita vya kutisha kwa miaka 6”. Hayo yalisemwa na Andrea Iacomini, Mwakilishi wa Unicefu, Italia.

Aidha alisema  nakusanyo ya fedha za uhamasishaji ni kununua blanketi na vifaha vingine vya  watoto wa huko Siria, hivvyo anawaomba Taasisi za kisiasa, mashirikana na vyama vingine vya kijammi , watu binafsi  na raia , kujitokeza kwa wingi kwa kusaidia watoto hao kwa siku hiyo ya Aleppo itakayofanyika 22 Desemba 2016.

Aidha taarifa  kutoka  Umoja wa Mataifa , Ban Ki Moon alisema kuwa mshikamano wa kibinadmu utatue changamoto za jamii, kwani ukosefu wa usawa ufukara na ukosefu wa ajira ni miongoni mwa mambo yanayohitaji mshikamno katika kuyatatua.
Aliyasema hayo katika ujumbe wake kwa siku ya kimatafa ya mshikamano wa kibinadamu 19 Desemba 2016.

Ban alisema licha ya mafaniko ya maendeleo ya kibinadamu kwa miongo miwili iliyopita, changamoto hizo zinapaswa kutatuliwa kwa mshikamano ili kuziba pengo katika kuhakikisha maendeelo endelevu.Na pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni ubaguzi unaoendelea kuwa kikwazo katika ujenzi wa jamii jumuishi, pamoja na mabadiliko ya tabianchi yanayotajwa kuathiri zaidi wale ambao hawakuyachangia kwa kiwango kikubwa.
Bwana Ban Ki Mooni alitoa msisistizo wa jukumu la mshikamano wa kibinadamu katika kujenga maisha ya utu kwa wote katika sayari dunia.

 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.