2016-12-20 15:07:00

Kardinali Nzapalainga kusimikwa rasmi heshima ya jina la Mtakatifu Andrea della Valle


Kardinali kusimikwa  Rasmi Heshima ya jina la  Mtakatifu Andrea della Valle.
Jumapilia 18 Desemba , Kardinali Dieudonné Nzapalainga  Askofu Mkuu wa Bangui  wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alisimikwa rasmi heshima ya jina la Mtakatifu Andrea della Valle.


Ni Parokia ya Kanisa Katoliki  mojawapo la   mjini Roma lenye  msimamizi wa Mtakatifu huyo, ambapo ni utamaduni wa Vatican kwa  kila anayepewa Ukardinali, kupewa jina la heshima ya   mtakatifu  ambaye ni msimamimizi wa Kanisa mojawapo  mjini Roma.  


Kardinali Nzapalainga alipokelewa na   Gombera wa Kanisa hilo Padre Carlos Gómez Ruiz ambaye baada ya kuingia Kanisani aliletewa msalaba na kubusu kwa heshima ikiwa na maana ya kulipokea jina rasmi la msimamizi wake wa Kanisa hilo.


Baada ya kuwasalimia waumini, alianza ibada ya misa Takatifu. Katika  ibada hiyo alikuwepo hata mwakilishi wa Katibu wa Umoja wa Mataifa, kiongozi mkuu ya operasheni ya Umoja wa Mataifa katika nchi ya Jamhuri  ya Afrika ya Kati , Onanga-Anyanga Parfait,  na  Mkuu wa Ulinzi wa Vatican Domenico Giani.

 

Sr Angela Rwezaula.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.