2016-12-20 14:44:00

Balozi wa Papa Nchini Ukrain kutembelea Jumuiya za kikatoliki Ukraine


Ubalozi  wa Vatican nchini Ukraine, ulitoa  taarifa  kwamba  Balozi wa Vatican nchini Ukraine , Askofu Mkuu Claudio Gugerotti   alitembelea jamuiya za kikatoliki na ya Kanisa  lenye liturujia ya kigiriki huko Donetsk na Luhansk  kuanzia 16 -18 Desemba 2016, pamoja na ziara yake katika jumuiya mbalimbali za dini  zikiwa katika maandalizi ya sikukuu,   aliwafikishia salamu na baraka kutoka kwa  Baba Mtakatifu Francisko. Balozi wa Papa aliwahi kutembelea Jumuiya za Zaporizhzhia na  Donetsk mapema Aprili mwaka huu wakati wa sikukuu ya Pasaka.

Wakati wa mkutano  na Jumuiya hizo, Balozi  alizungumzia kuhusu shughuli za Papa Francisko anazofanya bila kuchoka kwaajili ya amani katika ulimwengu na shahuku yake ya kujisikia  kuwa miongoni mwa watu duniani kwa ajili ya kuwaonesha ushirikiano na mshikamano wake. Aidha katika fursa  la Ziara yake ya Luhansk, Balozi pia alitembelea mji wa  Mytrofan ya Luhansk na Alchevsk,  kuona makao ya  Idara ya Mahusiano ya nje ya Kanisa la kiotodosi la  Ukraine. Katika ziara  yake  Balozi  alifuatana na msaidizi Askofu wa Jimbo Kuu  Katoliki la Kharkiv na Zaporizhzhia la Kanisa Katoliki inayoshughulikia miji miwili iliyotajwa.

 

 Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.