Jumamosi 17 Desemba 2016 Baba Mt.Francisko Alikutana na wanajumuiya ya Nomaldelfia
mjini Vatican nakuwaeleza, anayo furaha ya kukutana na kutaka kujua uzoefu wa Jumuiya
yao, na kwamba alishangazwa juu ya ushuhuda wao.
Katika hotuba yake aliwaeleza , kipindi cha majilio kinatusaida kutafakari juu ya
maajabu ya Mwana wa Mungu aliyekuja kwa njia ya mwili na katika kuzaliwa kwake ameleta
mwanga na amani duniani.
Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana ni kuonesha Mungu aliye juu na ambaye anatawala ulimwengu
nni yule aliyejinyenyekeza katika udhaifu wa mtoto. Aliendelea, hii inatufundisha
tusijiweke mbele zaidi ya wengine , bali tumeitwaa kujishusha na kuwa wadogo ili
kuwahudumia wengine walio wadhaifu. Na hii ni kusema kwamba kama Mungu mwenyewe kwa
njia ya mwanaye alikuja duniani kama binadamu tulivyo sisi ila hakuwa na dhambi ni
sawa na kusema , kwa maneno yake Yesu , “chochote mlichowatendea wadogo mmenitendea
mimi” (Mt, 25,40).
Papa aliendelea mwanzilishi wenu Padre Zeno Saltini alitambua hayo , lakini pamoja
na matatizo aliyokutana nayo alikwenda mbele kwa matumani, kwa lengo la kupeleka
mbegu ya Injili hata katika sehemu zenye zenye ugumu wa kupokea.Akaongeza; na aliweza!
Kwasababu hiyo Jumuiya yenu ya Nolmadelfia ni mfano huo. Padre Zeno leo hii anawakilisha
mfano wa imani ya kitume kwa Kristo na ameigiza mwalimu wake ambaye ni Mungu. Na
huyo anaendelea kuinama kwa watu wanoteseka, wadhaifu na masikini wa mwisho.
Hivyo ushuhuda wake, uwaongoze kila siku katika kutoa matunda ya wema na kupanda
mbegu inayoongozwa na upendo wa kiinjili , na kwa uaminifu wa Kanisa.
Aliwakumbusha tena maneno ya Yesu, ya kuwa “ kuwalisha wenye njaa, kuwavalisha walio
uchi , kuwapokea masikini kati ya watu, ni sawa na kupokea na kumpenda Mwana wa Mungu,
bali atakaye fanya kinyume na hayo atakuwa kama asemavyo Mt. Yohane ya kuwa kama
umpendi ndugu yako unaye muona , unawezaje kumpenda Mungu usiye muona(1Yh 4,20).
Alimalizia hotuba yake kwa wanajumuiya hiyo ya Normadelfia akisema, ndugu kaka na
dada urithi wenu wa kiroho , unahusiana kwa namna ya pekee na maisha ya kindugu,
yenye sifa hasa ile ya ukarimu kwa watoto na kutoa huduma kwa wazee. Ninawatia moyo
wa kuwapa mifano jamii juu ya huduma hiyo muhimu. Ya watoto na wazee kwajili ya kujenga
maisha yao ya baadaye kwa watu; kwani watoto wataendeleza mbele historia yao, na
wazee kwasababu wao, utoa uzoefu na hekima ya maisha yao.
Papa alisisitiza ya kwamba wasichoke kamwe kuendeleza majadiliano haya kati ya vizazi
, na kulifanya neno la Mungu kuwa ndiyo msingi wa maisha kamili ya kila siku. Kwa
namna hiyo mtakuwa mfano wa karibu wa Mungu kati ya watu nakuweza kuzitambua nyuso
za wale wadhaifu ya kwamba ni mfano wa mtoto yesu. Na aliwatakia sikukuu njema wote
ya kuzaliwa kwa Bwana na kuwabariki
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |