2016-12-19 13:41:00

Hati za Utambulisho za Balozi wa Korea nchini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, siku ya Jumatau tarehe 19 Disemba 2016, amepokea Hati za utambulisho ya Balozi wa Korea nchini Vatican, Prof. Jonghyu Jeong, ambaye alizaliwa tarehe 26 Novemba 1950 na ana mke na watoto watatu. Bwana Jeong alihitimu shahada ya sheria katika chuo kikuu cha Chonnam nchini Korea mnamo mwaka 1976, na baadae shahada ya uzamifu kwa fani ya sheria katika chuo kikuu cha Kyoto nchini Japan mnamo 1987.

Kati ya nyadhifa mbali mbali alizowahi kuhudumia ni pamoja na kuwa mkufunzi katika vyuo vikuu kama vile Chonnam nchini Korea, Munich Ujeumani, Kyushu na  Hitotsubashi nchini Japan, na mjumbe wa kamati ya maadili ya kibaolojia ya Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Korea. Mwaka 2010 alikuwa mjumbe maalumu wa Rais wa Jamhuri ya Korea mjini Vatican.

Na Padre Celestine Nyanda

Idhaa ya Kiswahili, Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.