2016-12-17 17:05:00

Papa asema tuangalie nyuma na kufanya kumbukumbu ya historia yetu


Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 17 Desemba 2016, ameadhimisha Ibada ya Misa akiwa na Makardinali wanaoishi mjini Roma kwenye Kanisa dogo la Mtakatifu Paulo mjini Vatican kama sehemu ya maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 80 tangu alipozaliwa. Katika mahubiri yake alichambua akisema ni nini maana ya kufanya kumbukumbu , zaidi  juu ya mandalizi ya kumpokea Bwana aliye karibu na hasa Kanisa linapoanza maadhimisho ya Novena kwa ajili ya maadhimisho ya Siku kuu ya Noeli inayobisha hodi mlangoni! Alisema ni nini maana ya kusema kwamba tusimame kidogo wakati ni kipindi  cha kutafakari kwa kina, jibu ni kwamba Papa alisema, Kanisa linataka tufanya kumbukumbu. Simama, na fanya kumbukumbu. Tazama nyuma tuangalie  mwendo,ni kumbukumbu.Ni tabia ya masomo  kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu ya  Torati inatia moyo na nguvu.

Kumbukumbu inayotolewa katika maandiko yenyewe inakazia , namna yak usali na kukutana Mungu, kwa kama vile maneno yanayoanza “Kumbukeni wakubwa wenu…”tunayokutana  nayo katika Barua kutoka kwa waebrania.”Iteni kumbumbukumbu  siku ya kwanza”. Baadaye katika sehemu hiyo , tunasoma , kundi la mashahidi katika sura 11  ilitoa njia ya kufika na  kutimiliza siku za nyakati. Aliendelea, “ Fanyeni kumbukumbu na angalieni nyumba  ili  kwenda mbele”  hiyo ndiyo maana ya siku ya leo” : neema ya kumbukumbu : Papa alisisitiza , ni kuomba neema hiyo: na siyo kusahau!

Ni hakika upendo , na msisahau ni upendo daima uwekwe   mbele ya macho yetu ,na akaongeza , kwa wema wake  tulipokea, hakika  ni  upendo wa kuangalia Historia: tunatoka wapi , baba zetu, babu zetu, na njia ya imani…Na kmbukumbu hiyo inatusaidia , kwasabababu inatufanye tuwe makini katika kusubiri ujio wa Noel inayotazamiwa. Kukumbuka ndiyo kiini cha uchaguzi wa watu: Yesu Kristo, Mwana wa Daudi , Mwana wa Ibrahimu.Ni taifa lililochaguliwa kutembea katika ahadi na nguvu ya agano , na maagano mengine ambayo yalifuata. Ndiyo nia ya Kristo na ndiyo njia yetu: Papa alisema ni rahisi. Tuliahidiwa  akasema tembeeni kwenye uwepo wangu na adilifu  kama alivyo Baba.

Ahadi itakayotimia  mwisho wake ,Agano hilo linatufanya  tutambue ya kwamba wote tumechaguliwa, uchaguzi na agano ni kama mihimili ya kumbukumbu ya kikristo. Na hiyo ndiyo maana ya  kuangalia nyuma ili kuweza  kwenda mbele.Leo hii ni neema : Papa alisema tunaposikia maneno ya Injili ni kufanya kumbukumbu na kusikiliza sura hiyo , kuna historia ya neema  kubwa , na vilevile historia ya dhambi. Njiani tunakumbana na neema na dhambi. Papa alikumbusha ya kwamba “ katika historia ya ukombozi kumekuwa na dhambi kubwa ! Akaongeza , katika orodha , kuna hata watakatifu. Hata sisi katika maisha yetu  tuko  kama wao: kwani kuna kipindi cha imani kubwa kwa Bwana na  ya furaha ya huduma, na wakati mwingine kuna kipindi kigumu cha ukosefu wa  uaminifu, ni dhambi inayotufanya tujisikie mahitaji ya kukombolewa.

Na hii  ndiyo hakika, kwasababu , tunapokuwa na hitaji la ukombozi, tunafanya kitubio kwa imani na kufanya maungamo ya imani “ mimi ni mdhambi lakini we unaweza kuniokoa, Wewe unaweza kunipeleka mbele. Ndiyo hivyo kwenda mbele na furaha ya matumaini. Tulianza majilio katika njia ya kusubiri kwa shahuku Bwana na leo tutazame , nyuma, tuangalie kama safari hiyo ilikuwa nzuri , ambayo bwana hatudanganyi, kwani  Bwana ni mwaminifu.Pia tutazama tupo katika historia na kwa maisha yetu njia hiyo  imekuwa nzuri na ya uamininfu, au  kama imekuwa mbaya ya dhambi. Lakini Bwana yupo pale, na mkono wake ameuinua  juu kutusimamisha na kusema nenda mbele!Na ndiyo maisha ya kikristo,: nenda mbele ukutane naye wakati  mtimilifu. Ni mwendo wa kina , unahitaji kukesha na kumsubiri Bwana,  lakini tusipungikiwe na neema ya  kumbukumbu ya kuangalia nyuma kwa yale yote aliyotutende Bwana , kwaajili ya Kanisa na  historia ya ukombozi,na kwa njia hiyo tutambua kwanini Kanisa linatutaka tusome sehemu hiyo hata kama inaonekana  kuwa nzito, lakini kuna Historia ya Mungu aliyetaka kutembea na watu wake, na mwisho wake  ni  , mwanadamu kama sisi. 

Na Bwana atusaidie kuanza upya neema ya kumbukumbu, lakini ni ngumu , nzito, kuna matatizo mengi, japokuwa  mwandishi wa Waraka kwa waebrania anayo sentensi nzuri dhidi ya malalamiko yetu  akisema: “kaa kwa utulivu, kwasababau hajafikia kuleta damu” ni sentensi ya kuchekesha , lakini kwa mwandishi huyo anatusaidia kwanda mbele,. Na Bwana atupatie neema hiyo.

Sr. Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.