2016-12-16 14:41:00

Salam za matashi mema kwa Papa Francisko kutoka Afrika!


Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM kwa niaba ya familia ya Mungu Barani Afrika, linapenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko anapoadhimisha kumbu kumbu ya miaka 80 tangu kuzaliwa kwake hapo, Jumamosi, tarehe 17 Desemba 2016. Familia ya Mungu Barani Afrika, inamshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kusimama kidete: kulinda, kutetea na kudumisha Injili ya familia na kwamba, SECAM kwa upande wake, itaendelea kujizatiti kwa ajili ya kutangaza, kudumisha na kushuhudia tunu msingi za maisha ya ndoa na familia.

Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar  kwa mara nyingine linamtakia heri, baraka na maisha marefu Baba Mtakatifu Francisko katika utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. Aendelee kutekeleza dhamana na majukumu yake kwa uaminifu, uadilifu, imani, mapendo na matumaini. Ujumbe wa SECAM umeandikwa Askofu Emmanuel Adetoyese Badejo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, CEPACS.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.