2016-12-16 16:40:00

Ratiba elekezi wakati wa Kipindi cha Noeli na Mwaka Mpya 2017


Idara ya Liturujia za Kipapa imetoa kalenda elekezi ya maadhimisho ya Ibada za misa  ya Baba Mt. katika sherehe za siku kuu ya Noel 2016 na kwa  Mwaka mpya 2017. Misa ya mkesha wa Noel  tarehe 24 Desemba 2016 itaanza saa saa 3.30 za usiku  wanaombwa Kardinali, Patriarki, maaskofu wakuu , maaskofu wanaopenda kadhimisha misa na baba Mt wafike saa 2.45 Usiku katika Kanisa dogo la Mt. Sebastiano ndani ya Basilika ya Mt. Petro.
Na mapadre ambao wanataka kuadhimisha na baba Mt. Wakiwa wawe  na ruhusa iliyotolewa katika ofisi ya kiliturgia ya Baba Mt. na wafike saa 2:00 usiku kwenye sehemu ya  mkono wa Costantino ili kuvaa mavazi matakatifu.  
Makardinali , Mapatriaki , Maaskofu wakuu, maaskofu ma  wengine wenye ruhusa ya uwepo kwa mujibu wa Vatican na wanataka kuudhuria misa bila kiadhimisha , wanatakiwa wavae nguo zinasostahili na wafike saa tatu katika altare ya kitubio , ili kupata nafasi za kukaa watakazoelekezwa na wahusika wa liturjia.    

25 DESEMBA 2016 : KUZALIWA KWA BWANA

25 Desemba 2016 Misa Takatifu ya Noel itaadhimishwa na Baba Mt, na saa 6 mchana mbele ya Basilika ya Mt Petro atatoa ujumbe wa Noel na kutoa Baraka ya «Urbi et Orbi» kwa dunia nzima.

31 DESEMBA 2016

31 Desemba 2016 saa 11 za jioni  Baba Mt. atasali masifu ya jioni ya vijilia ya sikuu ya Bikira Maria mama wa Mungu ,yakitanguliwa na kuabudu Ekaristi Takatifu  wakati wa kufunga mwaka na atawapa  Baraka kwa Ekaristi Takatifu.
Mapadre ,  wote watakaopenda kuhudhuria maadhimisho hayo wanatakiwa wavae nguo zao na wote wakutane pamoja saa 10:30 Jioni  mbele ya altare ya kitubio kwaajili ya kupewa nafasi na waandaji liturjia.

1 JANUARI 2017: SIKUKUU YA BIKIRA MARIA MAMA WA MUNGU NA SIKU YA KUOMBEA AMANI DUNIANI

Tarehe 1Januari 2017 Baba Mt. Ataadhimisha Misa Takatifu ya Bikira Maria mama wa Mungu ikiwa ni siku ya nane ya Noel, ambayo inakwenda sambamba na Siku ya Amani Duniani ikiwa na kauli yake mbiu “. Kutotumia nguvu: mtindo wa siasa ya amani".
Makardinali, Patriaki Maaskofu wakuu na maaskofu watakaopenda kuadhimisha na Baba Mt. wanatakiwa wafike saa 3:15 Asubuhi katika Kanisa dogo la Mt. Sebastiano kwenye Basilica ya Mt. Petro  kwa mavazi matakatifu  tayari kwa ibada Takatifu ya Misa.
Na Mapadre watakaoudhuria wakiwa na ruhusa kutoka  ofisi ya liturgia ya Vatican wafike saa 3 katika sehemu ya Mkono wa Constantino  kwa mavazi matakatifu.
Waliobaki kwa mujibu wa Kanisa la vatican kama wanapendelea kufika bila kuvaa mavazi ya kiliturgua  Kardinali, Patriaki , Askofu wakuu , maaskofu na wengine wakutane mbele ya Altare ya Kitubio saa 3.30 asubuhi kwa maelekezo y anafasi za kukaa.

6 JANUARI 2017 : SIKUKUU YA EPIFANIA

Tarehe 6.Januari 2016 Misa ya sikukuu ya  Epifania itaadhimishwa na Baba mtakatifu  katika Basilica ya Mt. Petro saa 4:00 asubuhi .
Kukutana kwa wote wanaopendelea kuadhimisha ibada kuu na Baba Mt.ni saa 3:15 kwa upande wa Makardianli, Patriaki, Maaskofu wakuuu na maaskofu na wengine, katika Kanisa dogo la Mt.Sebastiano tayari kwa mavazi matakatifu ya Ibada.
Na wengine wanaotakata kuudhuria bila kuadhumisha misa wanatakiwa wafike saa 3:30 katika Altare ya kitubio ili waonyeshwe nafasi za kukaa.
Mapadre wafike saa 8.30 , upande wa mkono wa Costantino ndani ya Basilika ya Mt. Petro kwa mavazi matatifu tayari kwa Ibada Takatifu.

Waliobaki kwa mujibu wa liturjia  la vatican kama wanapendelea kufika bila kuvaa mavazi ya kiliturjia  Kardinali, Patriaki , Askofu wakuu , maaskofu na wengine wakutane mbele ya Altare ya Kitubio saa 3.30 asubuhi.
Utaratibu huo umetolewa Na Mwalimu wa Liturgia za kipaa.
Mons. Guido Marini.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.