2016-12-15 16:38:00

Walimu wa Sheria walikwenda kuona Yohane kwa mbali kuhukumu na siyo kubatizwa


Wachungaji wanasema ukweli lakini wanawapokea watu kwa kile wanachoweza kutoa, hiyo ni hatua mojawapo, kinachosalia  Bwana atafikiria, ni ujumbe wa Baba Mt. Katika mahubiliri ya asubuhi 15 Desemba 2016 katika Kikanisa kidogo cha Mt. Martha Vatican.
Akichambua Injili ya siku  kuhusu utume wa Mt Yohane mbatizaji alisema; wote walikuwa wanakwenda kumuona,  hata wafararisayo, na walimu wa sheria, lakini kwa mbali yaani kuhukumu na siyo kwa kubatizwa.Katika Injili ya siku Yesu anauliza umati walikwenda jangwani kuona nini, mwanzi unaotikiswa na upepo, mtu aliye vaa mavazi maridadi?


Siyo anaye vaa mavasi maridadi , kwamba wavaao mavazi maridadi wanaishi ki anasa katka majumba ya mfalme,Papa aliongezea kama katika nyumba za maaskofu.Yule mliyekwenda kumuona ni nabii,ni zaidi ni zaidi ya nabii, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko Yohane,nabii wa mwisho kwasababu baada ya yeye kuna Massiha , alieleza baba Mt.  Ya kwamba alikuwa mkubwa kwasababu Yohane alikuwa mwaminifu kwa yale aliyokuwa ameulizwa na Bwana, n mkubwa kwasababu ni mwaminifu alisistiza papa. Ukubwa wake unaonekana pia katika mahubiri yake
 
Alitumia maneno makali na mabaya kuwahubiri wafarisayo  walimu wa sheria, ma makuhani,hakuwaeleza wawe na mwenendo mzuri, bali aliwambia hivyo tu “enyi  kizazi cha nyoka”Hakuwa na lugha ya kulemba kwa maana walikaribia pale kwasababu ya kuangalia na kuchunguza , kamwe hawakufika kwa moyo ulio wazi  bali walikuwa ni kizazi cha nyoka, Papa alibainisha ya kamaba Yonahe , Maisha yake yalikuwa hatarini, lakini yeye alikuwa mwaminifu.
 Mfano mwingine alisema hata Erode alimwambia uso kwa uso “ mzinzi wewe hauruhusiwi kuishi njia hiyoya uinzi! Kutokana na maneno ya Yonane , Papa alitoa mfano ni leo hii hakika  kwamba iwapo Paroko katika mahubiri ya  Jumapili moja adhubutu kusema miongoni mwenu kuna baadhi ya vizazi vya nyoka  na kuna   wazinzi, kwa hakika , askofu wake atapokea barua za haraka zisemazo “ mtoe paroko hapa kwasababu ametututukana .Na Yohane lakini alikuwa akiwatukana, je  kwasababu gani? Papa aliendelea  ni kwasababu ya uaminifu  wa wito wake na katika ukweli.


Hata hivyo Papa alibainisha ya kwamba Yohane kwa watu wengine aliwambia mfano, watoza ushuru,watoze kwa haki wakinzia na kile kidogo. Vilevile aliwambia  maaskari  wasitoe vitisho au kukemea mtu yeyote na kwashauri  watoshe  na mishahara yao.Hii ina maana ya kutokujiingiza katika vitendo vya rushwa  katika dunia  hii, Papa alielezea  Askari akikusimamisha anapima kama umekumywa pombe na kuanza  majibishano ya hapa na pale....
Yohane alibatiza wenye dhambi , pamoja na hayo alijua amefanya kidogo maana alijua kwa ujio wa Bwana atafanya zaidi , na waliongoka. Ni mchungaji , papa alisema, aliyekuwa akitambua hali za watu na kuwasaidia wasonge mbele na Bwana . Yohani alikwa nabii mmoja tu ambaye alipata neema ya kuonyeshwa na Yesu.


Pamoja na kwamba Yohane alaikuwa mkubwa na nguvui ,vilevila uhakika wa wito wake lakini pia naye alipatwa na wakati wa kiza , na kuwa na  mashaka, Papa Franncisko alisema,Yonae alipkuwa amefungwa , alianza kuwa na mashaka hata kama alikuwa amembatzia Yesu, kwasababu alikuwa mkombzoi si kama alivyokuwa akimfikiria.Na ndipo aliwatuma wanafunzi wawili kumuuliza kama kweli yeye ni masiha.Yesu anasahihisha maono ya Yonahe kwa jibu la hakika, akisema mwambieni Yohane,  Vipofu wanapata kuona, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa .Hata wakubwa wanaweza kuwa na mashaka kwa sababu ni wakubwa alisema Papa; lakini kitendo cha wakubwa kuwa na mashaka ni jambo zuri pia zuri . kwasababu mara nyingine ufikiria wanao uhakika wa wito wao, japokuwa  inapotokea mara moja Bwana kuwaonyesha njia mpya ya kufuata, hapo mashaka hujitokeza.

 

Alitoa mfano Papa na kuendelea; lakini hiyo siyo hali halisi, ni uzushi, kwasababu siyo masiha niliyekuwa namtarajia.Shetani anafanya kazi hiyo na akisaidiwa na baadhi ya marafiki au siyo!Huo ndiyo ukubwa wa Yohane akiwa nabii wa mwisho kati ya kundi la waumini walioanzia na Ibrahim, ni yule anaye hubiri  toba  na aliye na maneno ya kulaani kiburi , lakini mwishowe alinguka katika   shaka , huo ni mpango mzuri wa maisha ya kikirsto. Kwa kifupi katika mahubiri yake alisema inabidi kusema mambo ya kweli na kuwapatia watu kile kinachowezekana kuwapatia


Na hivyo tumuombe Yohane neema na ujasiri wa kitume daima kusema mambo ya ukweli , kwa upendo wa kitume , kuwapokea watu na kuwapatia kile kiwezekanacho, ndiyo hatua ya kwanza, mengineyo Mungu atafanya yote, vile vile hata neema ya kuwa na mashaka, na hasa tunapofikia mwisho wa maisha yetu, maana kishawishi kinaweza ktujia na  kujiuliza kama ni kweli yote tuliyo amini yapo hau ndiyo ndoto za kufikrika? Yaani kuwa na majaribu dhidi ya imani yetu,na  juu ya Bwana .


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.