2016-12-13 16:50:00

Bikira Maria ni kielelezo cha wanawake wanaopambana!


Imani ya Bikira Maria inaangazia jamii kipofu mbele ya waliobaguliwa, na ukiburi wa upofu wa wache, ni mahubiri ya Jumatatu 12 Novemba 2016 katika misa iliyofanyika kwa lugha ya kihispania  jioni katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wakati Kanisa linafanya kumbukumbu ya Bikira Maria wa Guadalupe msimamizi wa Bara la Amerika ya Kusini na Ufilipini.

Watu wengi kutoka Amerika ya Kusini na Ufilipini wanaoishi Roma, pia idadi kubwa ya makardinali, maaskofu , watawa na idadi kubwa ya viongozi wa Roma, walipata kuhudhuria , na baba mtakatifu, aliwaomba  waige mfano wa Maria na kuwatazama wengine kama vile mtazamo wake mama.
Mahubiri ya Baba Mtakatifu yalitokana na Injili iliyosomwa inayohusu Maria kumtembelea ndugu yake Elizabet, na wote wawili walikuwa wajawazito, baada ya kusikia  ya sauti ya furaha ya Elizabeth una heri wewe, wewe uliyesadiki” Lk 1,44-45) Imani ya Maria inaangaza jamii, ambayo mara nyingi inawaacha walio wengi na hasa wanye matatizo ,hawawezi kufikia yale mahitaji yao.

Ni jamii inayoendelea kujidai katika maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia, lakini pia imegeuka kuwa kipofu na kutokujali mbele ya maelefu ya sura zinazobaki nyuma kimaendeleo, watu wanaobaguliwa  ni kutokana na upofu wa walio wachache. Jamii hiyo inaishia  kujenga utamaduni  wa kujidanganya na dhiki, Baba Mtakatifu alitoa mfano ya kuwa ni  kama vile tumezoea kuishi na  jamii isiyo kuwa na imani. Akitazama mateso ya ulimwengu alinedelea; Ni jinsi gani ilivyo ngumu kijigamba katika jamii yenye uwezo, wakati tunatazama bara hapo akigusia bara la marekani  ya kusini anakotokea, alisema wamezoea  kutazama maelfu na maelfu ya watoto na vijana wako barabarani wanaomba omba na kusinzia kwenye vituo vya treni, kwenye maandaki ya vituo vya treni au mahali popote wanapopata nafasi.Aidha watoto na vijana waonya nyaswa na kunyonywa kwenye kazi ngumu na kulazimishwa kutafuta fedha kwa wapita njia, au kusafisha vioo vya magari kwenye magari yetu. Hawa watoto wanahisi ya kwamba hawamo ndani ya treni ya maisha, hawana nafasi.

Familia zenye kuwa na machungu alibainisha  Baba Mtakatifu , wakitazama watoto wao wanakufa , wanakuwa chanzo cha biashara ya kifo, ni jinsi gani ilivyo ngumu  kuangali jinsi ilivyogeuka kuwa jamb la kawaida  juu ya kubagua wazee na kuwafanya waishi kiupweke, au kutazama wanawake, watoto na vijana wanabugudhiwa. Hizi ni halia ambzo zaweza kupelekea wasiwasi wa imani yetu alisema Papa. Mbele ya hali hiyo wote tunapaswa kusema kama Elizabeth, heri wewe uliye sadiki , na kujifunza ile imani yake yenye  nguvu ya kuweza  kutoa huduma iliyo kuwa inafanana na inafanana na ya Mama yetu. 

Kufanya sherehe ya Maria ,hawali ya yote ni kufanya kumbukumbu ya Mama , ya kuonyesha sisi siyo yatima , tunaye Mama! Na mahali ambapo kuna mama daima kuna arufu ya nyumbani. Palipo na mama , ndugu wanaweza kugombana , lakini daima umoja utashinda. Mahali palipo na mama , hapatakosekana  na undugu.Alitoa mfano kuhusu Bara lake la Amerika ya kusini ya kuwa amekuwa akisataajabu akikumbuka wale mama wapiganaji , daima walipigana peke yaom na daima walikwenda mbele ili wapate kusaidia watoto wao.Hivyo Baba mtakatifu aliendelea naye Mama Maria yuko namna hiyo kwaajili yetu, ni mama anayetupigania  dhidi ya jamii isiyokuwa na imani. Kumtazama Maria ni kutukumbusha Bwana alikuja kututembelea na anapipita daima kwa wale wanaweza kufanyika mwili wa Neno lake, wanaoweza kufanyika mwili katika maisha yao na kugeuka kuwa ishala inayoonekana ya uhuruma yake.

Kwa njia ya tumbo la Bikira Maria Mungu ametutembelea , kama ilivyosikika katika wimbo mwingine wa Baraka na kwahiyo Mungu anakuja kukutana nasi na kubadili maisha yetu kuwa ya sifa. Maria ni mtume na mmisionari, anayekwenda nje kuembea kama vile mwaka 1531 huko Mexico  sehemu ya Tepeyac alimtokea  Juan Dieogo na kumuongoza kwa watu ma katika uamuz ya  watu waliokuwa wamejazwa na uchungum na yeye akawa mama yake na watu wote. Baba Mtakatifu aliwaomba wajifunze   imani hii kwa sababu  mama Maria ni ishala ya utume, mwanamke anayetambua kusindikiza, kusindikiza imani yetu katika hatua  mbalimbali. Uwepo wake utupelekea maridhiano, na kutupatia nguvu  ambayo uleta  mshikamano wa nchi yetu iliyobarikiwa ya marekani, na kusema ndiyo ya maisha na kukataa aina zote za ubaguzi, udanganyifu, wa watu au mtu.

Hatuna woga wakutoka kwenda kuwatazama wengine, mtazamo wetu uwe kama mtazamo wake, mzamo  huo unaotufanya tuwe ndugu , tuufanye kwa sababu Mtakatifu Juan Diego anajua ya kwamaba yupo mama , na tnatambua ya kwamaba tuko chini ya kivuli chake  cha ulinzi , ambacho ni chemichemi ya furaha yetu , na tupo katika mikono yake. Baba Mtakatifu Francisko alimahitimisha sala yake akisema: Utupatie amani na ngano , mama yetu na mtoto, nchi inayounganisha nyumba, Kanisa, na shule. Mkate uwe ni kwa aajili ya wote, na imani iwashwe kwa njia ya mikono yake, na macho yenye nyota yawaangazie wale wanaotembea katika gizaa!

Amina.

Sr Angela Rwezaula. 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.