Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 11 Desemba 2016 alikumbuka mashambulizi ya kigahidi iliyotokea Jumapili 11 Desemba, 2016 katika maeneo tofauti huko Cairo Misri ambapo mashambulizi yalifanyika katika Kanisa , Kanisa kuu la kikopti la mtakatifu Marko na kusababisha vifo vya watu na majeruhi, akisema ”Ni sehemu nyingi ambazo kwa bahati mbaya ni ghasia zinasababisha machafuko na kuleta vifo na uharibifu.
Jibu moja katika matatizo hayo ni Imani kwa Mungu, umoja katika maadili ya kibinadamu pamoja na ustaarabu. Aidha alitoa salam zake kwa watu wote na pia kuonyesha mshikamano na ukaribu kwa Papa Tawadros II na Jumuiya yake ya kikristo kutokana na shambulizi la Kanisa Kuu la Kikoptik na kusali kwa ajili ya wote waliopoteza maisha na majeruhi. Kufuatia na habari za shambulio la kigaidi huko Cairo inasadikiwa watu 25 kufa na hasa ni watoto na wanawake kwasababu wataalam wanasema bomu liliangukia sehemu inayokaliwa na wanawake wakati wa kusali ndani ya Kanisa Kuu la Mtaktifu Marko makao Makuu ya Patriaki wa kikopta Papa Tawadros II.
Naye waziri wa mambo ya ndani ya nchi Magdi Abdel- Ghaffar akikaririwa na Gazeti la
Asia , linasema walitembelea sehemu zote zilizoharibika, na kuona vipande vipande
vya madirisha ,na damu zilizokuwa zimatawanyika kila upande. Aidha wanasema Shambulio
la Jumapili ni mojawapo ya mashambulizi mazito yalitokea katika Jumuiya ya wakristo
wa Kikopta. Mara ya mwisho ilikuwa shambulizi ni lile la Januari 2011 huko Alessandria
lililosababisha watu 21 kupoteza maisha yao na 70 kujeruhia.
Aidha Papa aliwakumbuka waliotangazwa kuwa wenye heri, ni wafiadini 17 walio uwawa
huko Laos kati ya 1954 na 1970 na wanajeshi wa kikomunisti wa Patthet Lao, na kutangazwa
na Kanisa kuwa wenye heri Jumapili 11 Desemba huko Vientiane mji wa nchi huko kusini
mwa Bara la Asia . Kati yao kuna mmisionari mmoja Mario Borzaga kutoka nchini Italia
na wenzake 14 waliouwawa kutokana na kutetea imani yao wa Shirika la kimisionari
oblati wa Maria mkingiwa wa Asili .
Hivyo baba mataktifu alisema huo ni ujasiri na kuwatia moyo, uwe mfano kwa wamisionari
hasa hasa kwa makatekista katika sehemu za kimisionari ambao kazi yao ni tunu msingi
ambayo siyo rahisi kuoindoa, na Kanisa linawashukuru kwa mchango wao , aliendelea
” Makatekista wanafanya kazi nzuri tuwapigie makofi hao wanao peleka ujumbe wa Bwana
ili upate kukua ndani mwetu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |