2016-12-12 16:01:00

Kufurahi katika Bwana maana yake ni furaha ndani ya moyo


Katika Jumapili ya tatu ya Majilio, Baba Mtakatifu katika omelia yake wakati wa sala ya Malaika wa Bwana katika viwanja vya Mtakatifu Petro, aliwakumbusha   juu ya mafundisho ya barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi  juu ya kufurahi katika Bwana, na kwamba inahusu furaha ya kweli  ndani ya moyo.


“Siyo furaha ya kijujuu au ya muda tu,  ya kiulimwengu , au furaha ya kuchuma , hapana siyo hiyo bali ni furaha ya kweli na hakika  ambayo tunatakiwa kuigundua  radha yake, ni radha ya furaha ya kweli, ni furaha inayogusa moyo kiundani katika maisha yetu wakati tukisubiri ujio wa Yesu  amabo ukweija wajia  na kuleta ukombozi duniani, uliletwa na masiha aliyehaidiwa  kwa Bikira Maria kule Betlehemu.


  Katika  kitabu cha Nabii Isaya ujumbe wa  ukombozi uliotangazwa ni wa kufika kwa Bwana ambaye ubadili mambo yote na kufanya maisha ya binadamu kuwa mapya. Mungu alikuja katika historia ili kutukomboa kutoka utumwa wa dhambi, na akaweka hema kati yetu ili kushirikiana nasi  maisha yetu, kutuponya na majeraha na  kufunga madonda . Papa alikazia kuwa “Furaha ni tunda la tukio hilo la ukombozi na upendo wa Mungu”
“Baba Mtakatifu alibainisha ya kuwa wakristo wote tunaalikwa kuonja  msisimuko wa furaha , kwani Mkristo hasiye na furaha ,maana yake kuna   jambo linalomkosa, au siyo mkristo ! maana Mkristo ana  furaha ya moyo daima  , furaha  yenye msukumo wa ndani ambao umsaidia kuwa mjasiri. Bwana na atukomboe kutoka utumwa wa ndani na nje, atuongoze katika njia ya uaminifu, mapito na kukesha kwasababu atakaporudi ,atukute na furaha yetu kamilifu”. 


Noel iko karibu na inajionesha katika mapambo  barabarani, hata majumbani, vilevile  hata katika kiwanja cha Mtakatifu Petro wameweka pango.
Aliezea Baba Matakatifu kuwa  hizi ni ishala za nje zinazotualika kumpokea Bwana ambaye daima anakuja kubisha hodi , katika   milango yetu ya roho, kutukaribia, na kutukaribisha  tutambue mapito yake na yale ya ndugu zetu wanaotukaribia,hasa  wadhaifu na wahitaji.
mwisho Baba Mtakatifu  aliiomba kushirikishana na wengine furaha ya ujio ulio karibu wa mkombozi,ha hasa  kuwatia moyo  na matumaini masikini, wagonjwa, wapweke, na wale wasiyokuwa na furaha.

Vilevile Baba Mtakatifu akiwasalimia mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kwa namna ya pekee salama ziliwaendea watoto na vijana wa Roma waliofika  na sanamu zao za mtoto Yesu zitakazowekwa kwenye pango zilizotengenezwa ndani ya nyumbana kila mtoto aliyefika hapo alisikia ujumbe wa baba mtakatifu akiwaeleza kwamba watakapokuwa katika pango zao na wazazi wao , waombe mtoto Yesu awasaidie kupenda  Mungu na ndugu, na kuwakumbusha wasali kwaajili yake kama vile naye awakumbukavyo.

Umati wa Vijana, watoto na wazazi wao kutoka maparokia ya jimbo la Roma asubuhi ya Jumapili walisali misa ndani ya Basilika ya Mtakatifu Petro, misa iliyoongozwa na Cardianali Angelo Comastri , ambayo ni utamaduni wa Roma kubariki sanamu ndogo hizo za mtoto Yesu.
Papa alisema wakapokuwa katika pango zao  na wazazi wao, mwombeni mtoto Yesu awasaidie kupenda Mungu na jirani, na kumbuka  kumuombea Papa  kama anavyo waombea yeye.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.