Katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu , Shirika la habari al Sir linatoa ripoti ya kuwa tunaishi katika dunia ya masumbuko kwa upande wa kisiasa jamii na utamaduni. Daima watu hawajiamini , kutokana na msukosuko ambao uzaa hofu .Kutokana na tukio la siku ya kimataifa ya haki na amani iliyofanyika 10 Desemba 2106 huko Uswis, Muungano wa makanisa ya Uswis yametoa tamko kufuatia siku hiyo likisema linakumbusha nyenzo za kupambana na hali ya misukosuko na hofu ni haki ya binadamu, pamoja na kwamba siyo daima zinatekelezwa bali kila siku inabidi kupambania
Aidha katika habari hiyo ilielezea juu ya kuondoa sheria ya kifo kwa kudumisha usalama, na si hiyo tu bali maana yake ni kuondoa sheria ya kifo duniani na kudumisha haki katika huru na usalama ambao uwe uhuru wa mawazo na dini, haki kwa wahamiaji na wanao oomba makazi , kulindwa inapohitajika , kuondoa kwa nguvu katika nchi inapotakiwa , kuheshimu utaifa na tamaduni na dini,kwaajili ya maendeleo endelevu.
Vile vile waligusia juu ya ubaguzi, ya kwamba haki na amani inaamaanisha katika siku hiyo kurudia kwa upya majukuma yao na kukataa aina zote za ubaguzi ikiwa na maana ya ubaguzi wa aina nyingi kama vile utumwa mamboleo na aina zake zote kama chuki, matusi, yanayojitokeza katika mitandao ya kijamii na pia kutaadharisha kwamba kukubali makosa kwa upande wa baadhi ya watendaji wa jamii ndani ya mitandao ufungulia milango ya kutokovumiliana.
Na mwisho walisema Haki za binadamu "hazigawanyiki", wanakumbusha mashirika yote ni lazima kuhakikisha wanatunza utu "kwa watu binafsi na jamii": Kwasasa hali ya hofu inatutaka tuendelee mbele na ahadi zetu za uwajibikaji.
All the contents on this site are copyrighted ©. |