2016-12-08 15:30:00

Watawa wa Bikira Maria Immakulata na utume wao nchini Tanzania


Watawa katika maisha na utume wao ni mashuhuda na vyombo vya umoja, udugu na mshikamano kwa ajili ya huduma kwa Mungu na jirani. Ni watu wanaohimizwa kujenga moyo wa upendo na mshikamano na watu mbali mbali ili kuwasaidia wale wanaoteseka kutokana na ujinga, maradhi na umaskini sehemu mbali mbali za dunia. Sr. Maria Marximiliana Massawe katika mahojiano maaalum na Radio Vatican anazungumzia kwa ufupi historia, maisha na utume wa Shirika lake. Shirika la Masista wa Bikira Maria Immakula lililoanzishwa huko nchini Poland kunako mwaka 1884 limekuwa na kuenea sehemu mbali mbali za dunia na kwa miaka ya hivi karibuni limeingia nchini Tanzania katika majimbo ya Tunduru-Masasi, Mtwara, Jimbo kuu la Dar es Salaama pamoja na Jimbo Katoliki Same.

Hili ni Shirika la kitawa lililoanzishwa ili kuwasaidia na kuwahudumia wasichana na wanawake waliokuwa wanaishi katika mazigira magumu na hatarishi kwa maisha, utu na heshima yao kama binadamu walioumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Watawa wa Shirika hili wameendelea kusoma alama za nyakati na sasa maisha na utume wao unajikita katika sala na kazi; huduma makini kwa familia ya Mungu kwa njia ya kufundisha dini shuleni ma utume Parokiani kadiri ya mahitaji ya Makanisa Mahalia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.