2016-12-08 14:27:00

Tetemeko la ardhi Indonesia na watu wengi kupoteza maisha na wengine makazi yao


Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra ambapo majumba mengi yameporomoka na misikiti .Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limesema hakuna hatari ya kutokea kwa kimbunga. Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini. Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani mwendo wa saa 11:03 asubuhi saa za huko ,Jumanne 6 Desemba katika kina cha 17.2km (maili 11) chini ya ardhi.

Akiongea na waandishi wa Radio Vatican kuhusu  hali ya sasa ya Sumatra ni Matteo Amiggoni, muhusika wa Caritas Internationalis  Ufilipin na Indonesia  na kusema ,Wanahesabu watu 100 wamekufa na 70 ni majeruhi   wakiwa na hali mbaya.  Watu 1,500 ni kundi la kusaida kuokoa watu , na nusu ya hao ni wanajeshi , ambao kwa sasa wanaendelea na operesheni ya kutoa watu waliobaki ndani ya vifusi hivyo. Aidha taarifa zinasema, kwa bahati nzuri haikujitokeza tetemeko ndani ya bahari , maana mwaka 2004 ilitokea tetemeko ndani ya bahari ikasabaisha mafuriko yaliyopoteza maisha ya watu wengi.

Alimalizia akisema kuwa uzoefu walio nao juuya tukio hilo daima Caritas  hawaangalii rangi ya kitu chochote , wala ngozi wala macho wala mambo mengine , bali wanachojali ni kupeleka misaada mahali inapohitajika, na kwa upande wa kisiwa cha Indonesia wamejifunza hali hizi zinazojitokeza na hasa mara baada ya tukio la 2004.

 

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.