2016-12-07 15:25:00

Jumuiya ya Sant'Egidio kupewa hadhi ya uangalizi wa kudumu katika Baraza


Jumatatu 5 Desemba wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa 107 mjini Gineva wa Shirika la Kimataifa la Baraza la Uhamiaji  walipata kuwatunuku  rasmi hadhi mpya ya kudumu ya kuwa waangalizi wa wahamiaji katika Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) Jumuiya ya Sant’Egidio .Na walitia sahini ya Mkataba wa makubaliano ya kukuza utekelezaji wa shughuli za misaada mipya  kwa lengo la wahamiaji na wenye shida.

Ni kamati ya kwanza Tangu Shirika la Kimataifa lilipojiunga na mfumo wa Umoja wa Mataifa , ulioandaliwa kwaajili ya tukio la miaka 65 ya kuanzishwa kwa Shirika hili ambayo imekuwa na ongezeko zaidi ya nchi wanachama kwa sasa  166 na kuongez Jumuiya hiyo kwenye  wajumbe katika uangalizi wa kudumu.Hadhi Mpya ya Jumuiya ya Sant’Egidio ndani ya  Shirika la Kimataifa ilisindikizwa na maandishi ya  Mkataba wa Makubaliano , ambao ulitiwa saini 6 Desemba,2016  Mjini Gineva na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa Willian Lacy Swing na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Sant’Egidio  Giacomo Cesare Zucconi

Baada ya miaka ya ushirikiano na Jumuiya ya Sant’Egidio , wanayo furaha ya kushirikiana kati ya Shirika la Kimataifa na Jumuiya ili kuweza kuingia kwenye awamu mpya, alisema Federico Soda , Mkurugenzi wa Ofisi ya Uratibu wa Shirika la kimataifa la Baraza la uhamiaji kwa upande wa Mediterranean.

Mkataba wa Makubaliano unafafanua baadhi ya maeneo muhimu ya ushirikiano kati ya mashirika mawili, na hasa uendelezaji wa njia za kisheria,  kuingia kwa wahamiaji na wakimbizi ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za  kufanya ili kuwaunganisha na familia zao. Na makubaliano hayo ni muhimu katika kufungua vikwazo vya kibinadamu kwa wahamiaji wanaojikuta katika hali ya dharura.Hati hiyo pia inasisitiza umuhimu wa kuanzisha ushirikiano na  umoja wa wahamiaji na wakimbizi katika nchi zao asilia.

Naye Mauro Garofalo Mhusika wa mahusiano ya Kimataifa ya Jumuiya ya Sant’Egidio alisema kutambuliwa  kuwa waangalizi wa kudumu katika  Baraza la Kimataifa inawapa heshima na kuwapa msukumo mkubwa wa kuwajibika,na katika changamoto za kimataifa zinazokabili kutokana na wahamiaji na wakimbizi kuna haja ya ushirikiano kati ya Mashirika ya Kimataifa,na vyama vya kijamii. Ni matokeo ya mradi wa majaribio ya msaada wa kibinadamu, iliuyoundwa kwa harambee chanya kati ya vyama vya kijamii na Taasisi za Italia na kwa  sasa imefikia utafiti wa nchi nyingine za Ulaya.

Tangu Desemba 2015  , Jumuyia ya Sant’Egidio imeweza kuwa na makubalino na  nchi ya Italia katika  mradi wa majaribio juu ya ufunguzi wa misaada ya  kibinadamu kwa lengo la kuwasaidia watu wenye hali mbaya, kama vile wanawake na watoto, wazee , na watu wenye ulemavu au wenye magonjwa makuu, kuwahamisha kwa njia salama nchini Italia, na wengine wanaoomba hifadhi, Misaada hiyo  ya  kibinadamu inaanzia tangu kuwasili kwao, kwa miaka miwili wakimbizi elfu  na wengi wao ni kutoka Lebanon na sasa  wangine wanatoka Syiria wakikimbia vita.Hadi sasa watu 500 tayari wameshawasili  idadi hiyo itazidi kuongezesawa kufikia na 2017.

"Kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano na Jumuiya ya Sant'Egidio", alihitimisha Federico Soda, "ni kuingia tayari katika sehemu ya siasa ya  ushirikiano  kibinadamu ambao umekuwa sasa  thabiti ndani ya shirika lao,  ni  matarajio ya kuanzisha juhudi mpya  ambayo iweza  kutoa msaada na huduma  kwa wahamiaji zaidi na wakimbizi ".

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.