"Katika kukuza usalama wa nyuklia, Jumuiya ya Kimataifa inadhihirisha maadili na
wajibu, ili kukuza hali ya kuaminiana na kuimarisha usalama, vyama vya ushirika kwa
njia ya mazungumzo ya kimataifa" ni maelezo katika ujumbe wa Monsinyo Antoine Camilleri,
Msaidizi wa Katibu kwa Mahusiano na nchi za nje Vatican akizungumza katika Mkutano
wa pili wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia huko Vienna Austria mwezi huu.
Katika jumbe wake Monsinyo anaelezea juu ya mantiki ya hofu na kutokuaminiana katika
kuzuia nyuklia, alisema lazima kubadili mantiki mpya ya maadili ya kimataifa .Tunahitaji
maadili ya uwajibikaji , mshikamano na ushirikiano wa usalama wa kutosha na kazi ya
kuweka chini uthibi wa nguvu katika teknolojia ya nyuklia.
Kwa mujibu wa Monsinyo Camilleri anasema, vitisho kwa usalama wa nyuklia ni changamoto
kubwa kitaalam na kidplomasia na kwa kujibu hilo ni muhimu kushughulikia miendendo
mipana ya Usalaman siasa , uchumi, utamaduni ambayo uongoza hali na mashirika yasiyo
ya kiserikali katika kutafuta usalama , uhalali au nguvu katika silaha za nyuklia.
Vatican inaona umuhimu wa mkubwa kwa kuendeleza usalama wa nyuklia , kwa madhumuni
ya kuimarisha utawala na wala siyo kuenea kwa upungufu wa silaha za kinyuklia, hata
kwa ajili ya kukuza teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani. Aidha Monsinyo anaonyesha
sehemu mbili zinazotakiwa kuongeza juhudi , ya kwanza ni ulinzi wa kimwili na wa
nyenzo za kinyuklia , kwani kushindwa kudhibiti kunaweza kuleta athari mbaya; pili
sehemu nyingine anaonyesha umuhimu wa kulinganisha vitisho vya ndani na kuzuia mashambulizi
dhidi ya data na miundo nyeti, ambapo inabidi kuongezeka ulinzi kuanzia ngazi za
usalama wa habari na kompyuta, kwa kuhifadhi siri za taarifa muhimu kwa usalama wa
nyuklia
.
Msaidi wa Katibu kwa Mahusiano na Nchi Monsinyo Camillieri alibainisha pia mafaniko
makubwa yaliyopatika katika kuimarisha usalama wa nyuklia , na kuwashukuru Shirika
la Kimataifa la Nishati na Nyuklia kwa juhudi zao kwa ppindindi chote cha miaka hii
, wakati huo huo alilisistiza kwamba sehemu kubwa ya mafaniko ya Shirika la Kimataifa
la Nishati linategemea dhamira ya nchi wanachama kufikia ahadi zao za kisheria na
kimaadili, na kusema “ majukumu ya nchi wanachama lazima kubaki na lengo la mjadala
wetu wetu”.
Na mwisho wa hotuba yake alimazia mwakilishi wa Vatika huko Vienna akiweka wazi kwamba
haiwezekani kufanya ndoto kuhusu uzito wa changamoto zinazokabili jumuiya ya kimataifa
, lakini kwasababu ya changamoto hizi Vatican inakubali kuunga mkono kwa msaada
kwaajili Shirika hilo.
Mkutano katika kupiga marufuki silaha za nyuklia unakwenda sambamaba na ujumbe wa
baba Mtakatifu Francis alipotembelea katika Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 2015
akiwataka kutafuta njia ya kufanya ili dunia isiwe na silaha za kinyuklia na kupiga
marufuku kiujumla hayo mabomu.
All the contents on this site are copyrighted ©. |