2016-12-05 14:52:00

Kongamano kuhusu mifumo endelevu ya chakula la "kunja Jamvi " Roma


Kongamano la kimataifa la siku mbili kuhusu mifumo endelevu ya chakula kwa ajili ya afya na kuboresha lishe, la “kunja jamvi” lilifanyika  Desemba 2-4 mjini   Roma Italia.Kongamano hilo liliwakusanya pamoja watunga sera, wabunge, wataalamu wa afya na lishe kutoka serikalini na sekta binafsi, wataalamu wa maendeleo na wadau wengine.  Liliandaliwa na Shirika la chakula na Kilimo duniani FAO, na Shirika la Afya ulimwenguni WHO.

 

Katika siku hizo mbili kongamano hilo lilitoa fursa ya kutathimini kwa kina jinsi gani mifumo ya chakula inaweza kubadilishwa na kutoa lishe bora kwa wote. Akizunguza wakati wa kufunga kongamano hilo mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva alisema;  "kuna mambo muhimu manne ya kuzingatia,moja ni kuhitajika kuchagiza haraka mabadiliko katika mifumo ya chakula na mazingira ili kuweza kukabiliana na aina zote za utapiamlo na kuchagiza lishe bora. Pili kuhitajika ahadi ya dhamira ya kisiasa katika ngazi ya kitaifa ili kufikia mabadiliko haya yanayohitajika ili lishe bora iwe ajenda ya taifa.


 Tatu  ni lazima kuwajengea  uwezo walaji kwa kuwapatia taarifa wanazohitaji ili kuchukua uamuzi kuhusu kuchagua lishe bora. Na nne ni kwamba mabadiliko ya tabianchi ni moja au hatari kubwa ambayo inakabili kwa hivi sasa na mbinu za kukabili zinapaswa kuchochewa na lishe bora". Alisema Jose Graziano da Silva Mkurugenzi Mkuu wa FAO.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.