2016-12-05 10:15:00

Balozi Mostafa Arrifi awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 5 Desemba 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Mostafa Arrifi, Balozi mpya wa Morocco mjini Vatican. Balozi Mostafa Arrifi alizaliwa tarehe 21 Januari 1963 ana mke na watoto wawili. Kunako mwaka 1991 alihitimu shahada ya uzamivu kutoka Chuo kikuu cha Mohamed wa kwanza huko Oujda.

Tangu wakati huo amebahatika kufanya kazi mbali mbali kama mfanyakazi wa serikali tangu mwaka 1993 – 2000. Baadaye, aliteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha mahusiano ya kijamii na masuala ya uchumi kwenye Wizara ya Fedha na Uchumi kuanzia mwaka 2006 - 2009. Akateuliwa kuwa Mshauri na Mkurugenzi wa uchumi na fedha kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2011. Kuanzia Mwaka 2012 hadi mwaka 2014 alikuwa ni Mkuu wa Itifaki kwenye Sekretarieti kuu ya Wizara ya Uchumi na Fedha. Kunako mwaka 2014 akateuliwa kuwa Mshauri kwenye Wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirkiano wa kimataifa, hadi wakati huu alipoteuliwa kuwa Balozi wa Morocco mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.