2016-11-28 15:22:00

Jumuiya ya Kimataifa inaomboleza kifo cha Komrade Fidel Castro!


Baba Mtakatifu Francisko anaungana na viongozi mbali mbali duniani kuomboleza kifo cha Kamanda Fidel Castro, kilichotokea Ijumaa, tarehe 25 Novemba 2016 huko Cuba. Baba Mtakatifu katika salama zake za rambi rambi alizomwandikia Rais RaĆ¹l Castro wa Cuba anasema, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa kaka yako, Mheshimiwa Fidel Castro Ruz, Rais mstaafu wa Cuba.

Baba Mtakatifu anapenda kutoa salam zake za rambi rambi kwa ndugu, jamaa na wananchi wote wa Cuba walioguswa na msiba huu mzito. Anapenda kutolea sala zake kwa ajili ya Marehemu Fidel Castro ili aweze kupumzika kwa amani. Rais mstaafu Fidel Castro atazikwa rasmi tarehe 4 Desemba 2016 baada ya kuhitimisha siku tisa za maombolezo ya kitaifa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.