2016-11-25 08:48:00

Jengeni utandawazi wa mafao ya wengi!


Kanisa linaguswa na jinsi nchi nyingi zinazoendelea zinavyoshiriki katika uchumi wa Dunia leo, hata hivyo linatambua pia kuwa nchi nyingi zinazoendelea bado zinapambana na changamoto nyingi katika ushiriki huo wa uchumi wa dunia. Yamewakilishwa hayo na Askofu kuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa, katika mkutano juu ya sera ya uchumi wa dunia hivi karbuni Jijini New York.

Askofu mkuu Auza anafafanua kuwa ni nchi hasa ambazo zipo nyuma kiuchumi zinazohitaji kubaki kuwa dira katika kutatua suala la uchumi ili kuepuka zisijekubaki nyuma kupita kiasi katika kufikia malengo ya maendeleo ifikapo 2030. Nchi hizi zinafaa kupewa kipaumbele na kuonekana kuwa sehemu ya kile Papa Francisko anakiita “utandawazi wa mafao ya wengi”, kwa kuepuka nchi zilizoendelea kila mmoja kujikita katika mambo yake binafsi.

Biashara ni muhimu sana ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kwa 2030. Hata hivyo nchi nyingi zinazoendelea katika kujihusisha na biashara na nchi za nje, zinajikuta zikikumbwa na kushuka kwa bei za bidhaa, na hivyo kuwa kikwazo kwa mipango yao kupambana na umaskini ili kuinua hali ya uchumi. Askofu Mkuu Auza anaendelea kusema kuwa, uhamishaji wa teknolojia, usambazaji wa viwanda, na uongezaji nguvu katika masoko mahalia zinabaki kuwa nyenzo za lazima katika kuepuka mtego wa usafirishaji hasara wa bidhaa.

Askofu mkuu Auza anatambua ulazima wa taarifa ya fedha ya kimatafifa kuhakikisha mafanikio ya uhakika katika kufikia malengo ya maendeleo ya 2030 bila kuiacha nchi yeyote nyuma. Udumifu wa madeni kwa nchi zinazoendelea utafaa iwapo malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 yatafikiwa kwa wakati. Zaidi sana, ni muhimu kuhakikisha kuwa jumuiya ya kimataifa inaepuka ukopeshaji unaokuwa mzigo kwa wananchi wa nchi zinazoendelea au kuwa kikwazo kwa maendeleo yao. Majadiliano juu ya madeni ya nje kwa nchi zinazoendelea yanapaswa kufikiriwa pamoja na athari za mabadiliko ya tabia nchi na athari za viwanda zilizosababishwa na nchi tajiri kwa nchi zinazoendelea. Deni hilo la mabadiliko ya tabia nchi linaunganishwa na myumbo wa biashara na athari za mazingira, na hata matumizi yasiyo uwiano ya maliasili za nchi husika kwa muda mrefu. Askofu mkuu Auza ametoa mwaliko wa kila mmoja kushiriki katika kuweka mazingira mazuri na kujali dunia, ambapo ni Nyumba ya wote.

Na Padre Celestine Nyanda

Idhaa ya Kiswahili, Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.