2016-11-23 16:17:00

COMECE: Haki jamii; ushirikishwaji, ajira na mapumziko Jumapili!


Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu katoliki Ulaya, siku ya Jumatatu tarehe 21 Novemba 2016, imetoa maoni yake juu ya mhimili wa Umoja wa Ulaya kuhusu haki jamii. Katika waraka wao wamezingatia uchumi jamii wa masoko, huku wakiwatia moyo umoja wa ulaya kutopoteza malengo yao ya mpango mkakati kufikia mwaka 2020: kukabiliano na ukosefu wa ajira, hali na mazingira ya wafanyakazi,  wakijenga kwa pamoja msingi imara wa uchumi na fedha.

Kamati ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Barani Ulaya imeweka wazi kukubaliana kwao na malengo ya mapendekezo ya mhimili wa haki jamii. Kwa upande mwingine, kamati inawaalika umoja wa ulaya kusimamia uwiano na mwendelezo wa sera wanazokubaliana nazo, na wakati huo huo kuchukua mwelekeo wa kushirikisha nchi zote za ulaya na sio tu wanachama 19 wa umoja huo. Maaskofu Katoliki Barani Ulaya wanawazitia moyo nchi za Ulaya kushirikisha wadau wote wa maendeleo na haki jamii, waheshimu na kulinda haki za muda stahiki wa kazi, siku moja ya juma kuwa mapumziko kwa wafanyakazi wote, na wamependekeza siku hiyo kuwa ni jumapili. Wamesisitiza kutafakari nafasi ya malezi endelevu, katika nuru ya ukweli kwamba, elimu na malezi ni mashine za kuiweka jamii katika ubora wake.

Na Padre Celestine Nyanda

Idhaa ya Kiswahili, Radio Vatican.

 
 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.