2016-11-20 10:34:00

Waraka wa "Misericordia et misera" wakabidhiwa kwa familia ya Mungu


Baba Mtakatifu Francisko baada ya maadhimisho ya kufunga Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu, ametia sahihi kwenye Waraka wake wa kitume unaojulikana kama “Misericordia et misera” yaani “Huruma na huzuni” kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu. Waraka huu umekabidhiwa kwa wawakilishi wa familia ya Mungu. Hawa ni Kardinali Luis Antonio Tagle, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Manila, Ufilippini.

Wengine ni Askofu mkuu Leo William Cushley wa Jimbo kuu la Saint Andrews ed Edinburg, Uingereza. Wamissionari wa huruma ya Mungu kutoka DRC na Brazil; Shemasi wa kudumu pamoja na familia yake kutoka Jimbo kuu la Roma; Watawa wawili kutoka Mexico na Korea ya Kusini. Ukoo mmoja kutoka Marekani; Wanandoa watarajiwa; wanawake wawili Makatekista kutoka Jimbo kuu la Roma na waamini wawili ambao mmoja wao ni mlemavu na mwingine ni mgonjwa.

Huruma ya Mungu inapaswa kuendelea kumwilishwa katika nyuso za huzuni sehemu mbali mbali za dunia. Itakumbukwa kwamba, Waraka huu “Misericordia et misera” unazinduliwa rasmi na Askofu mkuu Salvatore Rino Fisichella, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Ujinjilishaji mpya, Jumatatu, tarehe 21 Novemba 2016 hapa mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.