2016-11-12 15:44:00

Askofu Fridorin A. Besungu ateuliwa kuwa Askofu mkuu nchini DRC


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Fridolin Ambongo Besungu, O.F.M. Cap. kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mbandaka-Bikiro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Besungu alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Bokungu-Ikela, DRC na msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu mteule Besungu kuwa Msimamizi wa kitume wa Jimbo Katoliki la Bokungu-Ikela, DRC.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule alizaliwa kunako tarehe 24 Januari 1960 na baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 14 Agosti 1988. Tarehe 22 Novemba 2004 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bokungu-Ikela, DRC.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.