2016-10-19 12:50:00

Msumbiji ; yakumbuka kifo cha Samora Machel


Wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, wamekusanyika Maputo Msumbiji kwa ajili ya kushiriki katika wiki la kumkumbuka Rais wa kwanza wa Msumbiji, Hayati  Samora Machel aliyefariki dunia miaka 30 iliyopita. Kumbukumbu hii ilianza rasmi katika mnara wa Samora Machel wa Mbuzini Mpumalanga, Afrika Kusini, ambako mtoto wake Samora, Melanga Machel, ameomba upelelezi mwingine  ufanyike, juu ya kifo cha baba yake.  

Samora Michel alifaki dunia tarehe 19 Oktoba 1986, baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka wakati akitokea katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Afrika , uliofanyika Lusaka Zambia.  Ndege yake ilianguka katika milima ya Lebombo karibu na Afrika Kusini. Samora Machel aliliongoza Taifa la Msumbuji hadi kujipatia uhuru wake kutoka ukoloni wa Wareno mwaka 1975 .

Padre Pinto Cuna wa Jimbo Kuu la Maputo , akizungumzia urithi ulioachwa na Samora Michel, kwanza alimtaja Marehemu kuwa alikuwa ni kiongozi jasiri mpigania uhuru wa kweli  na aliuawa na maadui wa amani na haki. Na kwamba,  kumbukumbu ya kifo chake kwa kila mwaka ni wito unaowataka raia wote wa Msumbiji, kudumisha tunu za uadilifu, amani, haki , umoja  na uzalendo katika taifa lao la Msumbiji kwa matendo na si kimaneno. Na ndiyo maana raia wengi wa Msumbiji huumizwa na hali ya mtafaruko unaojitokeza kati yao. Ni lazima kila mmoja ahakikishe anajiepusha na vurugu za kisassa za kutumia silaha za moto na umwangaji wa damu. Kifo cha Samora kinawakumbusha raia wote kuishi kama kaka na dada wa taifa moja.

Na Mchungaji John Timba wa Kanisa la Ulimwengu la Ufalme wa Mungu, yeye anasema Samora Micehl hakupenda kuona raia wenzake wakiteseka . Alipenda kumwona kila mmoja kushiriki katika kazi kwa manufaa ya wote. Na hivyo , raia wote wa Msumbiji wanapaswa kuishi na uvuvio huu kutoka kwa Samora , kuishi kwa kuvumiliana licha ya kutofautiana kisiasa, kiimani kikabila  kama mtu binafsi na kama wamoja ktika taifa huru la kidemokrasia.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.