2016-10-18 15:02:00

Papa Francisko kutembelea Jimbo kuu la Genova, 27 Mei 2017


Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kutembelea Jimbo kuu la Genova, Jumamosi tarehe 27 Mei 2017 kadiri ya taarifa zilizotolewa mjini Vatican na kusambazwa na Kardinali Angelo Bagnasco, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Genova, Italia, baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, Jumapili, tarehe 16 Oktoba 2016, kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Lorenzo.

Kardinali Bagnasco ametumia fursa hii pia kuzindua maadhimisho ya shughuli za kichungaji Jimbo kuu la Genova kwa mwaka 2016-2017. Hija ya kichungaji ya Baba Mtakatifu Jimboni humo, itakuwa ni zawadi kubwa kwa familia ya Mungu, baada ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu. Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko itakuwa pia ni kilele cha maadhimisho ya Jubilei ya miaka 380tangu Bikira Maria alipotangazwa kuwa Malkia wa Genova kunako mwaka 1637.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.